Mwanamitindo na mtangazaji maarufu wa Kipindi cha Keeping Up With The Kardashians, Kim Kardashian.
Chicago, MarekaniMWANAMITINDO na mtangazaji maarufu wa Kipindi cha Keeping Up With The Kardashians, Kim Kardashian ameonesha furaha sambamba na kujivunia mumewe, Kanye West kutunukiwa shahada ya udaktari wa sanaa (PHD) katika Chuo cha School of Art Institute jijini Chicago.
Kanye West alipotunukiwa shahada hiyo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, staa huyo aliyekuwepo nchini Brazil
akikitangaza kitabu chake kiitwacho Selfish, alishindwa kuhudhuria
katika siku ya kutunikiwa mumewe na kuamua kuweka mapenzi yake kwa
kuandika;“Dkt. Kanye West!!!! Najivunia kuwa na wewe mpenzi na najua hata mama yako atakuwa anajivunia kwa hilo.”
Kanye na Kim walioona mwaka 2014 pande za Forte di Belvedere in Florence, Italia.
Post a Comment