Stori ya ishu ya ubaguzi Afrika
ikarudishwa kwenye headlines na matukio ya South Africa.. Xenophobia
ikachukua nafasi ya ripoti nyingi za habari kubwa Afrika kwa zaidi ya
mwezi mmoja, kwa sasa hivi ni kama hali imetulia japo sio kwa asilimia
100 !!
Wenyeji wanahofu kuendelea kuwepo Afrika
Kusini, hii imeripotiwa na kituo cha TV cha SABC Afrika Kusini, wageni
wengine 60 kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliamua kuanza safari ya
kurudi kwao ikiwemo Wamalawi.
Watu zaidi ya 100 walilazimika kurudi
kwenye nchi zao kutokana na kuanza kwa vurugu za mashambulizi ya wenyeji
wa South Africa waliokuwa wakiwafukuza wageni.. wengine waliuawa na
wapo waliojeruhiwa na kupoteza mali zao pia kutokana na mashambulizi
hayo.
“Nataka nirudi nyumbani kwa sababu huku hali sio nzuri.. wanatupiga, wanataka kutuua nimeona nirudi tu nyumbani“– Hassan Shalifa, mmoja ya raia wa kigeni waliokuwa wakijiandaa kuondoka South Africa.
Post a Comment