Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Video: Msharo & Man M (The Winner) - 'Bolingo Nangaye'

Msharo & Man M 'The Winner' - Bolingo Nangaye
Audio Producer: Abah.
Video Diector: Herry Kafuku.

VERA Sidika Ajibu Mapigo ya Huddah Monroe Kwa Kuweka Picha Hii ikionyesha Chuchu zake zilivyo

If these socilates are not posting nudes they are busy calling out each other online. Well it’s barely a week since Vera played therapist by asking Huddah to tone down on her cocaine after a photo her naked boobs surfaced online.
Vera has shared a similar photo but the difference between the two is that she covered them. Braless though. She might not be the first lady walking around braless but is this the in thing? The last time i checked these two were out travelling to outdo each other but the tables keep turning.

Tazama Picha za Mafuriko ya Wanawake Waliojitokeza Millenium Tower Kumsikiliza Lowassa, Wengi Wamekosa Nafasi na Kubakia Nje

Ni mkutano wa wanawake wa ukawa na mh lowasa hapa jengo la millenium TOWER Dar es salaam,hizi ni picha za awali,hizi ni picha za awali ambazo nimekuwekea hapa kutoka katika mkutano huo.LOWASA bado hajawasili hapa ila idadi ya wanawake waliojitokeza hapa ni wengi sana kiasi cha kutokutosha katika jengo hili na sasa watu wanasubiri hatma yao kama watahamisha mkutano au italazimu wengine kuwa wapole na kusubiri nje kidogo.
Picha kamili za tukio hili zitakujia baadae kadiri muda unavyozidi kwenda msomaji wetu









Baada ya Kufunguliwa Kamati Mpya ya Miss Tanzania yawekwa Wazi..Jokate Ndani....

Baada ya kufunguliwa kwa mashindano ya kumtafuta Miss Tanzania na Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA), Kamati ya Maandalizi ya Michuano hiyo imekuja na mikakati ya kurejesha hadhi na heshima ya mashindano hayo makubwa ya kusaka walimbwende nchini.


Katika kuboresha mashindano ya Miss Tanzania, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga leo ametambulisha mbele ya waandishi wa habari kamati mpya yenye wajumbe 12, ambayo itakuwa inaratibu mashindayo hayo kwa sasa.
Lundenga amesema kuwa kamati hiyo inayoanza kazi zake hii leo, itashughulikia mapungufu yote yaliyojitokeza na kurejesha imani ya wananchi kwa mashindano hayo ikishirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali pamoja na Basata.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulishwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jokate Mwegelo ametoa shukrani kwa niaba ya kamati yake kwa kuamininiwa kupewa jukumu hilo na kuahidi maboresho makubwa na mikakati endelevu ya kurejesha hadhi ya Miss Tanzania.

Kamati Mpya ya Miss Tanzania inaundwa na wajumbe wafuatao:

1.Juma Pinto – Mwenyekiti
2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti
3.Doris Mollel – Katibu Mkuu
4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati
5.Hoyce Temu – Mjumbe
6.Mohamed Bawazir – Mjumbe
7.Gladyz Shao – Mjumbe
8.Magdalena Munisi 0 Mjumbe
9.Shah Ramadhani – Mjumbe
10.Hamm Hashim – Mjumbe
11Khalfani Saleh – Mjumbe
12.Ojambi Masaburi – Mjumbe

Kwa upande wa Sekretariet tunao wajumbe 4 ambao ni:

1.Dr.Ramesh Shah
2.Hidan Ricco
3.Yasson Mashaka
4.Deo Kapteni

Tisa wafariki kwa moto Buguruni

Nyumba moja iliyoko maeneo ya Buguruni Malapa Manispaa ya Ilala Jijini Dar es salaam, imeteketea kwa moto na kusababisha vifo vya watu tisa. Mashuhuda wa Tukio hilo wamesema chanzo cha moto huo hakijajulikana, na mpaka sasa tayari miili mitano imeshatolewa.

Hatimaye UKAWA Wakubaliwa Kutumia Uwanja wa Jangwani Jumamosi hii Kuzindua Kampeni zao


Malalamiko ya vyama vinavyounda UKAWA ya kakatazwa kutumia uwanja wa jangwani kuzindua kampeni yameanza kufanyiwa kazi na tume ya taifa ya uchaguzi na  taarifa zilizotolewa na mkuu wa idara ya mawasiliano ya CHADEMA Bw.Tumaini Makene zimesema kuwa uzinduzi huo utafanyika kwenye uwanja huo kama ilivyokuwa imepangwa.
 
Bw.Makene ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa baraza la vijana la vyama  vinavyounda UKAWA na waandishi wa habari ambao pia viongozi hao wametumia  nafasi hiyo kuiomba tume ya uchaguzi kuwakemea viongozi na watendaji wa  serikali kufanya kazi za siasa kwa lengo la kukibeba chama tawala.

Viongozi hao wa vijana wamesema  hatua ya viongozi na watendaji wa serikali ya kujihusisha moja kwa moja na kampeni za  CCM huku wengine wakitumia rasilimali za umma  na vyombo vya dola kukandamiza vyama vya upinzani inathibitisha ukweli wa  malalamiko yao.
~Mpekuzi blog

Mbowe Akata Rufaa Mahakama kuu Dhidi ya Hukumu yake


Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe amekata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yake Julai, mwaka huu, na kumtoza faini ya Sh1 milioni baada ya kupatikana na hatia katika kosa la jinai.

Mbowe alitozwa faini ya Sh1 milioni au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kumshambulia mwangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu wa 2010 katika Wilaya ya Hai, Nassir Yamin.

Hata hivyo, Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na Mbunge wa Hai, alilipa faini hiyo na kuachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Hai.

Katika rufaa hiyo namba 33/2015, iliyofunguliwa na wakili Peter Kibatala, Mbowe anailalamikia mahakama iliyomtia hatiani kuwa ilishindwa kushughulikia hoja muhimu katika kufikia uamuzi huo.

Pia, Mbowe analalamika kuwa mahakama ilishindwa kupima ushahidi kwa usahihi na pia, ilishindwa kutilia maanani ushahidi wa mashahidi wa upande wa utetezi akiwamo yeye.

Mbowe analalamika kuwa mahakama ilishindwa kutumia msingi wa jukumu la kuthibitisha shitaka pale ilipoeleza kuwa mashahidi wa upande wa mashtaka walitoa ushahidi uliojitosheleza.

Kwa mujibu wa Mbowe, Mahakama hiyo ilitakiwa itumie dhana ya upande wa mashtaka kuwa unatakiwa uthibitishe shtaka bila kuacha mashaka, jambo ambalo halikufanyika.

Mkata rufaa huyo anailalamika pia mahakama hiyo ilishindwa kueleza sababu zilizoifanya ifikie uamuzi wake huo kama inavyoelekezwa katika sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (CPA) kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Kutokana na sababu hizo, Mbowe ameiomba Mahakama Kuu kuifuta hukumu iliyomtia hatiani, kurejeshewa Sh1 milioni alizolipa kama faini na apewe nafuu nyingine yoyote ambayo mahakama itaona inafaa.

Rufaa hiyo imepangwa kusikilizwa Septemba 2, mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Aishiel Sumari.

Picha: Mavazi ya Kiafrika yalivyo tikisa kwenye maonyesho ya 'Afropunk 2015' New York

Maonyesho ya mavazi ya Kiafrika 'Afropunk' kwa mwaka wa 2015 mjini New York yaliyo fanyika tarehe 23rd August 2015 ambapo kwanzia 2005 yamekuwa yakifanyika kwenye jiji hili. Tizama vile vazi la kitenge linavyopendeza.























MKAPA Anguruma Tena, LOWASSA Vizingiti Kila Kona, NEC Yashitukia Vyama Vya Siasa, + UKAWA Yafanyiziwa! (Audio)

Kama hukuwa karibu na radio yako asubuhi hii uchambuzi wa magazeti @CloudsFMutakuwa umekupita. Zimesikika kubwa za leo kwenye vichwa vya habari baadhi zikiwa..


Vyama vya Siasa mtegoni, ratiba ya kampeni ya zua mjadala… UKAWA wafanyiziwa wakwama kupata uwanja wa Jangwani, NEC yapiga marufuku kampeni za mikusanyiko,Lowassa vizingiki kila kona azuiliwa kutumia uwanja wa Jangwani.


Mkapa anguruma tena alibariki Lowassa kukatwa, mgombea Urais CCM John Magufuliarudisha matumani kwa Watanzania asema akipewa nafasi ya kuiongoza nchi atateua Serikali yenye Mawaziri watakao kuwa watendaji kazi na waadilifu.


Mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa kuongea na wanawake wa katika kongamano la Wanawake lililoandaliwa na BAWACHA ya CHADEMA leo… Walemavu wasema CCM wanawabagua, Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza kuzindua kampeni za uchaguzi tarehe 30 mwezi huu.


Sumaye awa guzo CCM, NEC yashitukia, yasema kila Chama kifuate ratiba watoa angalizo kwa vyama hivyo kufuata Sheria zinazohusiana na namna na utaratibu wa kufanya kampeni hizo.

Sauti ya uchambuzi wa magazeti kupitia #PowerBreakfast ipo hapa chini.

Video: Wanawake hawa walio oana nchini Tanzania, Wameishi kwa muda wa miaka 15 sasa



Wegesa na Nyanswi. Ni wanawake wawili kutoka kwa jamii ya Wakuria. Wameoana kwa miaka 15. Wajane wasio na mrithi wa kiume hawawezi kurithi mali. Wagesa alimuoa Nyanswi kama mkewe ili kutatua tatizo hilo. Nyanswi ana wavulana kwa hivyo anaweza kurithi kutoka kwa Wagesa.

 Wanandoa hao wana wavulana sita,waliozaliwa na ndugu za marehemu mumewe Wagesa. Utamaduni huu pia ni njia ya kuepuka ghasia za nyumbani. Asilimia sitini ya wanawake katika eneo hilo wameshuhudia ghasia za vita ama zile za kihisia.

-BBC

Lulu amhenyesha Mboto ukumbini

Haji Salum ‘Mboto akisaidia kulibeba gauni la Lulu.
DIVA wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ hivi karibuni amemhenyesha staa mwenzake wa filamu, Haji Salum ‘Mboto’ baada ya kumpa kibarua cha kulishika gauni lake lisiguse chini.
Tukio hilo lilitokea kwenye fainali ya shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT 2015) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo Lulu na Mboto walikuwa washehereshaji.
IMG_1779Katika hali iliyoonesha Lulu alikuwa ‘siriaz’ stejini alimsisitizia Mboto kila mara ahakikishe amelishika gauni lake vizuri na asiliachie.
“Mboto hapa kazi yako ni kulishika gauni langu kwa nyuma kila nitakapokuwa nawe na ole wako uliachie,” alisikika Lulu ambapo Mboto alitekeleza ombi la Lulu.

Ukweli wa viumbe waishio angani, -4

Aliens wadaiwa kutinga Ikulu ya Marekani!
Wiki iliyopita niliishia pale nilipokuwa nikielezea muunganiko wa Aliens na makundi ya wanasayansi wa Marekani ambao wamekuwa wakielezwa kuwa huingia mikataba mbalimbali ya kubadilishana teknolojia na uvumbuzi wa teknolojia mpya. Mfano ni ile Teknolojia ya Aliens Software. SASA ENDELEA…
Katika kuchimba juu ya viumbe hao na nikushauri msomaji wangu kuwa na utamaduni wa kujifunza vitu vipya kila siku hasa vile ambavyo havipo kwenye utaratibu wa maisha yetu ya kila siku, itakusaidia kujua vitu kwa manufaa yako binafsi.
Kuhusu Aliens, inaelezwa kwamba, kwa bahati mbaya, mikataba ya wanasayansi hao wa Marekani na Aliens huwa na masharti mengi mabaya ambayo yanamuathiri na mengine yameshamuathiri moja kwa moja binadamu na bado inasadikiwa kuwa madhara mengine yanakuja. Wapo wasioamini lakini wengine wanaamini huo ndiyo ukweli.
Mwaka 1952, nchini Marekani kuliibuka utani kuwa Aliens walitua rasmi ikulu ya nchi hiyo kwa lengo la kuingia mikataba mbele ya rais wa wakati huo, Harry Truman. Ndivyo umma ulivyoaminishwa na wataalam wa propaganda.
Pia kitendo cha UFO kuonekana huko Washington, Marekani katika kipindi hichohicho, ndipo watu wakaanza kukubaliana na uvumi uliokuwa umeenezwa kuwa Aliens, UFO na wanasayansi wa Marekani walikuwa wana uhusiano.
Uwepo wa mawasiliano hayo ulitikisa Marekani ikiaminika kuwa ndiyo mwanzo wa uvamizi wa viumbe hao duniani. Usiku mmoja, mnara wa rada ya Uwanja wa Ndege wa Washington ulinasa vifaa visivyojulikana ambavyo vilikuwa vikikatiza angani kwa kasi ya ajabu kisha vikaelekea moja kwa moja kwenye Ikulu ya Marekani (White House).
Wakazi wa jirani na eneo hilo walishuhudia vitu kama baluni za rangi za njano vikidondoka kutoka angani. Vitu hivyo vilikuwa na mikia. Muda mfupi baadaye rubani mmoja alishuhudia UFO saba zikirandaranda angani.
Baadaye anga lote lilijazwa na vitu hivyo vilivyo-kuwa na mwanga mkali. Vitu hivyo vilishu-hudiwa na macho ya watazamaji hivyo ule uvumi sasa ukageuka habari ya kweli.
Wakati hayo yakiendelea, kuliibuka habari za mauaji ya kimbari huko Amerika ya Kusini. Ilielezwa kuwa mauaji hayo ya kutisha yalifanywa na hawa Aliens. Hata hivyo, baadaye ilisemekana kuwa shetani alikuwa ametembelea Amerika ya Kusini. Swali ni je, watu walitambuaje kuwa ni shetani?
Ilibidi kurudi kwenye maandiko juu ya uumbaji wa mbingu na nchi ili kujua kama Mungu alimuumba shetani?
Biblia inasema kuwa Mungu aliumba malaika wengi sana. Lusifa alipend-eza zaidi ya malaika wengine lakini kiburi kilimwingia, akaasi. Alifanikiwa kushawishi theluthi moja ya malaika wote na wote walifukuzwa kutoka mbinguni (shetani alianguka kutoka mbinguni kama mwanga wa radi (Luka 10:18).
Mbingu ni dunia ya roho (spiritual world) sayari kama Dunia, Mars, Jupiter na nyingine ni ulimwengu wa kuonekana. Kwa kawaida binadamu hawezi kuona dunia ya roho ila akifunguliwa macho ya roho ataona.
Hapa duniani tunaongozwa na hisia tano tu, sight, smell, hearing, taste na touch (au feel). Hiyo ndiyo maana binadamu anaongozwa na muda na nafasi. Kwa mfano, huwezi ukapenya kwenye ukuta au kupaa angani kama ndege. Hebu fikiria tu kuwa na uwezo wa kunusa au kuona sauti!
Itaendelea wiki ijayo, usikose.

Siri 4 matusi ya Diamond kwa Diva

Loveness Malinzi ‘Diva’
NI mtifuano! Agosti 24, mwaka huu ilikuwa siku mbaya kwa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ au baba Tiffah na mtangazaji anayekimbiza kwa sauti tamu hewani, Loveness Malinzi ‘Diva’ kufuatia kupishana lugha ndani ya studio za redio na hivyo, Diamond kumvurumishia matusi mwenzake.
Kupishana kauli huko kuliashiria kuwepo kwa uhasama wa siku nyingi kwa wawili hao huku kila mmoja akiwa anaamini mwenzake ana makosa na ndipo siri tano za Diamond kumtusi Diva zikajulikana.
MCHEZO ULIVYOANZA
Siku hiyo majira ya saa 9:00 alasiri, Diamond alitia timu kwenye studio za redio hiyo zilizopo Mikocheni, Dar kwa lengo la kumtambulisha msanii wake mpya kutoka studio yake ya Wasafi Records iliyopo Sinza-Mapambano, Dar.Mwanyeji wa Diamond alikuwa mtangazaji Hamis Mandi ‘B12’. Lakini ndani ya studio hiyo alikuwepo Diva.
platnumz
Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ au baba Tiffah.
ALIANZA DIAMOND
Kabla Diamond hajaanza kumtambulisha msanii wake, alianza na Diva kwa kumsema kwamba amekuwa akimchoresha mitandaoni kwa kumchafua.
DIVA AKAJIBU
Diva alijibu kuwa, kisa cha yeye kumchoresha, aliwahi kumuita Diamond kwenye Kipindi cha Ala za Roho lakini staa huyo hakutokea wakati meneja wake, Salam alimpa taarifa, akakubali na yeye Diva akaanza kutangaza mitandaoni kuwa, siku moja atakuwa na Diamond hewani jambo lilimfanya wasikilizaji wake kusema aliwaongopea na wengine kuanza kumtusi mitandaoni.
DIAMOND ACHAFUA HALI YA HEWA
Baada ya maneno hayo ya Diva, ndipo Diamond apoonesha dalili ya kukasirika na kutoa lugha ya matusi ambayo haiandikiki gazetini lakini akimaanisha kuwa, kama Diva angewahi kuwa mpenzi wake, angemheshimu.
MANENO BILA MPANGILIO
Diva naye alijimjia juu Diamond kwa kumwambia kuwa, hana hadhi ya yeye kuwa mpenzi wake, maneno ambayo yalimchefua baba Tiffah na kuanza kutupiana maneno bila utaratibu hali iliyomlazimisha B12 kuingiza matangazo ili kuwatoa hewani wawili hao.
Baada ya sitofahamu hiyo, Amani lilichimba na kubahatika kuibuka na siri nne (4) zilizomfanya Diamond kumtukana Diva.
SIRI YA KWANZA
Kwanza inadaiwa kuwa, meseji za Diva kwenye mitandao kumsema Diamond kwa kitendo chake cha kutotokea kwenye Kipindi cha Ala za Roho zilimfanya mzazi mwezake, Diamond, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kumbana baba wa mtoto wake huyo akimtaka aseme ukweli kama kuna siri iliyofichika kati yao
“Diamond amekuwa akimkatalia Zari kuwa, hakuna siri wala uhusiano wake na Diva. Kwenye kipindi hicho kama Diamond angekwenda, ilikuwa aongozane na Zari maana alikuwa hajajifungua. Diamond akawa anamwona Diva kama ana lengo la kuvuruga mapenzi yao.
SIRI YA PILI
“Kitendo cha Diva kutumia mitandao kumshambulia, Diamond alikiweka moyoni na kuahidi siku wakikutana laivu atampasulia ya moyoni mwake liwalo na liwe. Hata alipokwenda studio jana (Jumatatu), hakujua kama angekutana na Diva.”
SIRI YA TATU
“Diamond aliamini kuwa, Diva kumshambulia mitandaoni alilenga kumshushia heshima mbele ya jamii ili kumuua kisanii. Maana yeye mwenyewe alisema anaamini maneno ya Diva kwenye mitandao kuna zaidi ya kitendo chake cha kutotokea studio,” kilidai chanzo chetu.
SIRI YA NNE
Kwa upande wake, Diamond alipozungumza na Amani alianika siri ya nne akisema:
“Yule Diva dizaini f’lani kama ananitaka vile lakini mimi simpi nafasi ndiyo maana anatengeneza bifu na mimi.”
DIAMOND ANAENDELEA
“Diva amekuwa akinisema mara kwa mara. Mimi nilikwenda pale kwa lengo lingine, yeye akaanza kuleta zake za kuleta. Kila nikiitafuta sababu siioni. Sijawahi kumkosea popote pale.”
DIVA TAYARI KWA MWANASHERIA WAKE
Amani lilimtafuta Diva juzi kwa lengo la kumsikia anasemaje kuhusiana na sakata hilo ambapo alisema:
“Hii ishu iko kwa wanasheria wangu (tayari kwa kumpeleka Diamond mahakamani). Amenidhalilisha sana kama mwanamke nisiyefaa katika jamii. Ushahidi upo kila kona kwenye mitandao.”
ATISHIWA KUPIGWA, MAISHA
“Akaenda mbali zaidi na kutaka kunipiga maana lugha ya matusi haikutosha. Amenitishia maisha jambo ambalo halitakiwi kisheria. Hakuna aliye juu ya sheria. Sitazungumza zaidi.”
Imeandaliwa na Musa Mateja na Nyemo Chilongani.
© Copyright 24hours
Back To Top