Wiki iliyopita niliishia pale nilipokuwa nikielezea muunganiko wa Aliens na makundi ya wanasayansi wa Marekani ambao wamekuwa wakielezwa kuwa huingia mikataba mbalimbali ya kubadilishana teknolojia na uvumbuzi wa teknolojia mpya. Mfano ni ile Teknolojia ya Aliens Software. SASA ENDELEA…
Katika kuchimba juu ya viumbe hao na nikushauri msomaji wangu kuwa na utamaduni wa kujifunza vitu vipya kila siku hasa vile ambavyo havipo kwenye utaratibu wa maisha yetu ya kila siku, itakusaidia kujua vitu kwa manufaa yako binafsi.
Kuhusu Aliens, inaelezwa kwamba, kwa bahati mbaya, mikataba ya wanasayansi hao wa Marekani na Aliens huwa na masharti mengi mabaya ambayo yanamuathiri na mengine yameshamuathiri moja kwa moja binadamu na bado inasadikiwa kuwa madhara mengine yanakuja. Wapo wasioamini lakini wengine wanaamini huo ndiyo ukweli.
Mwaka 1952, nchini Marekani kuliibuka utani kuwa Aliens walitua rasmi ikulu ya nchi hiyo kwa lengo la kuingia mikataba mbele ya rais wa wakati huo, Harry Truman. Ndivyo umma ulivyoaminishwa na wataalam wa propaganda.
Pia kitendo cha UFO kuonekana huko Washington, Marekani katika kipindi hichohicho, ndipo watu wakaanza kukubaliana na uvumi uliokuwa umeenezwa kuwa Aliens, UFO na wanasayansi wa Marekani walikuwa wana uhusiano.
Uwepo wa mawasiliano hayo ulitikisa Marekani ikiaminika kuwa ndiyo mwanzo wa uvamizi wa viumbe hao duniani. Usiku mmoja, mnara wa rada ya Uwanja wa Ndege wa Washington ulinasa vifaa visivyojulikana ambavyo vilikuwa vikikatiza angani kwa kasi ya ajabu kisha vikaelekea moja kwa moja kwenye Ikulu ya Marekani (White House).
Wakazi wa jirani na eneo hilo walishuhudia vitu kama baluni za rangi za njano vikidondoka kutoka angani. Vitu hivyo vilikuwa na mikia. Muda mfupi baadaye rubani mmoja alishuhudia UFO saba zikirandaranda angani.
Baadaye anga lote lilijazwa na vitu hivyo vilivyo-kuwa na mwanga mkali. Vitu hivyo vilishu-hudiwa na macho ya watazamaji hivyo ule uvumi sasa ukageuka habari ya kweli.
Wakati hayo yakiendelea, kuliibuka habari za mauaji ya kimbari huko Amerika ya Kusini. Ilielezwa kuwa mauaji hayo ya kutisha yalifanywa na hawa Aliens. Hata hivyo, baadaye ilisemekana kuwa shetani alikuwa ametembelea Amerika ya Kusini. Swali ni je, watu walitambuaje kuwa ni shetani?
Ilibidi kurudi kwenye maandiko juu ya uumbaji wa mbingu na nchi ili kujua kama Mungu alimuumba shetani?
Biblia inasema kuwa Mungu aliumba malaika wengi sana. Lusifa alipend-eza zaidi ya malaika wengine lakini kiburi kilimwingia, akaasi. Alifanikiwa kushawishi theluthi moja ya malaika wote na wote walifukuzwa kutoka mbinguni (shetani alianguka kutoka mbinguni kama mwanga wa radi (Luka 10:18).
Mbingu ni dunia ya roho (spiritual world) sayari kama Dunia, Mars, Jupiter na nyingine ni ulimwengu wa kuonekana. Kwa kawaida binadamu hawezi kuona dunia ya roho ila akifunguliwa macho ya roho ataona.
Hapa duniani tunaongozwa na hisia tano tu, sight, smell, hearing, taste na touch (au feel). Hiyo ndiyo maana binadamu anaongozwa na muda na nafasi. Kwa mfano, huwezi ukapenya kwenye ukuta au kupaa angani kama ndege. Hebu fikiria tu kuwa na uwezo wa kunusa au kuona sauti!
Itaendelea wiki ijayo, usikose.
Post a Comment