WASANII ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameandaa Tamasha kubwa kuzunguka nchi nzima kwa pamoja na kukinadi chama hicho tawala pamoja na Sera zake ili kiweze kushinda Uchaguzi Mkuu onaotarajia kufanyika Oktoba Mwaka huu (2015).
Tamasha hilo litakalojulikana kama “MAMA ONGEA NA MWANAO 2015″
limeandaliwa na baadhi ya wasanii makada wa CCM wapatao 250 ambao
watazunguka mikoa zaidi ya 10 kukipigia kampeni chama hicho tawala ili
kiweze kupewa ridhaa tena na Wananchi ya kuendelea kuongoza nchi.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari
Mwenyekiti Msaidizi wa tamasha hilo, Wema Sepetu alisema madhumuni ya
tamasha la Mama Ongea na Mwanao 2015 ni kulinda mazuri yote yalioasisiwa
na CCM kupitia viongozi wake akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu Julias
Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume.
Msanii Sepetu akiyataja masuala hayo yalioasisiwa na CCM kupitia
viongozi hao kuwa ni pamoja na amani na utulivu uliopo hadi sasa,
maendeleo ya kijamii na kiuchumi yalioletwa hadi sasa, masuala ambayo
yanastahili kuendelezwa na wala si kubezwa.
Tamasha hilo linajumuisha wasanii kama Odama, Davina, Wastara Juma,
Keisha, Wellu Sengo (Matilda), Bi. Mwenda, Mama Lolaa, Mama Nyamayao,
Herieth Chumila, Thea, Maya, Chuchu Hans, Steve Nyerere pamoja na
wasanii wengine wengi.
Aidha alisema kupitia tamasha hilo wasanii hao pamoja na wenzao
watazunguka katika mikoa zaidi ya 10 kwa pamoja kufanya kampeni kumnadi
mgombea wa urais kupitia CCM, Dk. John Pombe Magufuli, mgombea Mwenza,
Samia Hassan Suluhu pamoja na viongozi wengine ngazi mbalimbali
wanazogombea kupitia chama cha Mapinduzi.
Madhumuni ya tamasha la Mama Ongea na Mwanao 2015 ni kulinda mazuri
yote yalioasisiwa na CCM kupitia viongozi wake akiwemo Baba wa Taifa
Mwalimu Julias Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume ambayo bila amani
mama awezi kujifungua salama, Bila mama hakuna familia, amani
inapotoweka mama hawezi kukimbia kilometa kadhaa na kuiacha familia
yake, bila mama hakuna ujasiliamali, mama ni kimbilio la baba, kaka,
dada na watoto…ikumbukwe kuwa mama ndio mpiga kura ndio maana tunasema
mama ongea na mwanao,” alisema Wema Sepetu.
“Na leo hii kuanzia sasa tunatambulisha kampeni yetu tunayoifanya
kuhamasisha vijana, kinamama, kinababa, mashabiki wetu wale wote wenye
sifa za kupiga kura wapige kura kwa kumchagua kiongozi bora anayetoka
Chama Cha Mapinduzi…chagua Dk. Magufuli, Samia Suluhu, wabunge na
madiwani wa Chama Cha Mapinduzi,” alisema Sepetu.
Aidha wasanii hao wamempongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwa kuongoza vizuri vikao vyote
vya chama hicho hadi kupatikana kwa mgombea bora wa urais kupitia chama
hicho (Dk. Magufuli), hivyo kuwataka wanaCCM wote ambao waligombea na
hawakupata nafasi kuungana na kukitumikia chama.
“…Mimi Wema Abraham Sepetu nikiwa na baadhi ya wasanii wenzangu ambao
tuligombea tunasema muda bado tunao na siku tunazo kwa kukitumikia
chama tukipewa ridhaa kwa njia yoyote na kwa nafasi yoyote ndio maana
hatuja teteleka tupo imara kuwatumikia wananchi katika nafasi nyingine
ndani ya CCM,” alisema Sepetu.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mratibu wa Tamasha la MAMA ONGEA
NA MWANAO 2015 litakaloipigia kampeni CCM, Steve Mengele a.k.a Steve
Nyerere akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha hilo.
Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015
litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu (kulia) akizungumza na
wanahabari jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao.
Kutoka kulia ni Wellu Sengo (Matilda) na Yobnesh Yusuph (Batuli).
Mwenyekiti Msaidizi wa Tamasha la MAMA ONGEA NA MWANAO 2015
litakaloipigia kampeni CCM, Wema Sepetu akizungumza na wanahabari jana
jijini Dar es Salaam juu ya tamasha na kampeni zao. Kulia ni Yobnesh
Yusuph (Batuli) na kushoto ni Steve Mengele a.k.a Steve Nyerere wakiwa
katika mkutano huo.
Post a Comment