Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameapishwa jana, siku sita kabla ya tarehe rasmi kulingana na katiba ya nchi hiyo ambapo alitarajiwa kuapishwa mnamo tarehe 26 mwezi Agosti.
Taarifa
kutoka ofisi ya Rais imesema Nkurunziza ameapishwa rasmi jana kuwa rais
wa nchi hiyo kwa muhula mpya wa miaka mitano ijayo. Sherehe hiyo ya
kuapishwa kwa kiongozi huyo wa Burundi imekuja ghafla na kutangazwa saa
chache kabla ya sherehe yenyewe kufanyika.
Maofisa
wa kijeshi waliagizwa jana asubuhi kuvalia sare zao rasmi na kufika
bungeni kwa ajili ya sherehe hizo za ghafla za kuapishwa kwa Rais
Nkurunziza. Hakuna viongozi kutoka nchi za kigeni ambao wamealikwa
kuhudhuria sherehe hizo za kuapishwa kwa kiongozi huyo wa Burundi.
Nkurunziza
mwenye umri wa miaka 51 ambaye ni kiongozi wa zamani wa waasi na
aliyekuwa mwalimu wa michezo, aliingia kwanza madarakani miaka kumi
iliyopita mwaka 2005 alipochaguliwa na bunge na kuchaguliwa na umma
mwaka 2010.
Muhula
wa tatu wa Nkurunziza umesababisha ghasia nyingi, kwa mujibu wa katiba
ya Burundi, rais anastahili kukaa madarakani mihula miwili tu ya miaka
mitano, lakini Nkurunziza na washirika wake wamedai muhula wake wa
kwanza madarakani, alichaguliwa na bunge na sio umma na kwa hivyo
anastahili kuendelea kuwa madarakani.
Uamuzi
wake mwezi Aprili mwaka huu kuwa atagombea muhula wa tatu madarakani
umezua mzozo mkubwa wa kisiasa na kusababisha ghasia nchini humo.
Nkurunziza
alishinda muhula wa tatu baada ya uchaguzi wa rais uliofanywa tarehe 21
mwezi Julai ambao ulisusiwa na vyama vya upinzani nchini humo na mapema
mwezi huu alitangazwa na tume ya uchaguzi nchini Burundi CENI kuwa
mshindi kwa asilimi sitini na tisa ya kura zilizopigwa dhidi ya mpinzani
wake wa karibu Agathon Rwasa ambaye licha ya kuususia uchaguzi huo
alipata asilimi 18 ya kura zilizopigwa.
Umoja
wa Mataifa, Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Marekani zimesema
chaguzi zilizofanywa nchini Burundi hazikuwa za huru na haki kwani
mazingira hayakuwa salama na bora kuendesha chaguzi na kuhakikisha kila
upande unashiriki kikamilifu.
Baraza
la usalama la umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya
kisiasa na kiusalama katika taifa hilo dogo la Afrika Mashariki na kutoa
wito pande zĂnazozana Burundi kufanya mazungumzo ili kuutatua mzozo huo
na kuepusha taifa hilo kutumbukia katika vita.
Watu
kadhaa mashuhuri nchini humo wametorokea nchiza kigeni wakihofia
usalama wao na wengine waliosalia nchini humo wamelengwa kwa kuuawa,
kushambuliwa, kukamatwa, kuteswa au kutishiwa maisha yao wakiwemo
maafisa wa kijeshi,wanahabari na wanaharakati wa kutetea haki za
binadamu.
Milio
ya raisasi imekuwa ikisikika karibu kila siku katika mitaa ya mji mkuu
wa Burundi, Bujumbura huku askari na wanajeshi wakijaribu kuwakandamiza
wanaompinga Rais Nkurunziza.
Mzozo
huo wa Burundi unahofiwa kuwa huenda ukalitumbukiza taifa hilo tena
katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kama vilivyoshuhudiwa kati ya mwaka
1993 hadi mwaka 2006 ambapo kiasi ya watu laki tatu waliuawa.
Post a Comment