KIKOSI
cha Kutuliza Ghasia (FFU) juzi kiliwatawanya Wafuasi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) na kumtia mbaroni mtu mmoja wakati wa msafara wa mgombea
ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Antony Mavunde ukielekea Ofisi za CCM
Wilaya.
Hali
hiyo ilijitokeza baada ya wanachama na wafuasi wa chama hicho kukaribia
ofisi za Wilaya na kuonekana kuwa yalikuwa maandamano ambayo yamezuiwa
kufanyika wakati wa wagombea kurudisha fomu. Yalijitokeza malumbano kati
ya askari wa FFU na wafuasi wa CCM ambao walisisitiza kwamba walikuwa
wakienda ofisi za chama.
Hata
hivyo FFU waliwataka watawanyike kabla ya kumpiga mmoja wa wanachama,
Mussa Idoha na kisha kumpakia kwenye gari la Polisi na kuondoka naye.
Askari
hao ambao walikuwa kwenye magari mawili ilibidi waondoke na kada huyo
na ndipo wananchi walipoamua kuandamana kwenda kituo kikuu cha Polisi
kabla ya kutulizwa na viongozi wao.
“Mgombea
ubunge wa Chadema alipokuwa akienda kuchukua fomu kulikuwa na
maandamano makubwa ya magari na pikipiki lakini sisi wameamua
kutukimbiza na kumpiga mmoja wetu,” alisikika mmoja wa wafuasi wa chama hicho.
Akizungumza na wananchi hao, Mavunde alisema kilichotokea ni faida kwao kwani wameiona nguvu ya CCM.
Aliwataka wananchi kutokubali kuwa wanyonge au sehemu ya kuchochea vurugu kwani walifuata taratibu zote za kisheria.
“CCM
tunatakiwa kuwa kielelezo cha amani, wafuasi wa CCM walizuiwa na polisi
lakini hakuna aliyetoa maneno ya kejeli na CCM itaendelea kuilinda
amani,” alisema na kuongeza:
“Sheria
haikuvunjwa, maelezo ya Polisi yanasema walizuia watu kutembea kwa
miguu walikuwa wakitaka msafara wa magari tu lakini tulipokuwa tunapita
njiani, watu walianza kujitokeza wenyewe na ikawa ni vigumu kuwazuia.”
Awali,
akizungumza baada ya kuchukua fomu, Mavunde aliwataka wananchi wa
Dodoma kumchagua ili washirikiane kutatua changamoto zinazoikabili
jamii.
Post a Comment