![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjXzkaLSG9TdWpIvBb3bdfiM7krGegUCSwPR0a4VWO42nST87pLKXNJUraKgeo_-XbQMvBBTLICVEbTE1_oKKPCBoUkCaQYJyOzKrYw2-bGOmo12Pa69rMkpmXa3rSzusby63u_mcWy7jQ/s640/OLU.jpg)
Gor Mahia chini ya kocha wake Frank Nuttal mpaka
kufikia hatua ya fainali, imecheza jumla ya michezo sita, ikiwemo michezo minne
katika hatua ya makundi, robo fainali na nusu fainali,
ambapo imeweza kushinda
michezo mitano na kutoka sare mchezo mmoja.
Mshambuliaji wa Gor Mahia,Michael Olunga anaongoza kwa
ufungaji, akiwa amepachika mabao matano, akifuatiwa na nahodha wa Khartoum
Salehdin Osman na msadizi wake Amin Ibrahim wote wenye mabao manne kila mmoja.
Kwa uapnde wa Azam chini ya kocha wake Stewart Hall,
imefanikiwa kufika hatua ya fainali bila ya kuruhusu nyavu zake kutikisika, huku
safu yake ya ushambuliaji ikiwa imepachika mabao tisa (9) katika michezo mitano
iliyocheza kuanzia hatua ya makundi.
Kuelekea mchezo wa Fainali, Azam FC iliziondosha Yanga
SC kwa mikwaju ya penati (5-4) hatua ya robo fainali, na kasha kuindoa KCCA
hatua ya nusu fainali kwa kuifunga kwa bao 1- 0, bao lililofungwa na
mshambuliaji chipukizi Farid Musa.
Mshambuliaji Kipre Tchetche ana mabao matatu kwa
upande wa washambuliaji wa Azam FC, akifuatiwa na nahodha John Bocco na Farid
Musa wenye mabao mawili kila mmoja.
Katika fainali hiyo ya kesho, inatarajiwa kuwa ya vuta
ni kuvute kutokana na makocha wa timu hizo, Frank Nuttal wa Gor Mahia kutaka
kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 tangu Gor Mahia
kushinda kombe hilo mara ya mwisho mwaka 1985 walipotwaa kwa mara ya tano (5).
Huku Stewart Hall akiwania kuweka historia ya kwanza
kwa klabu ya Azam FC kuweza kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza tangu
kuanzishwa kwa klabu hiyo miaka tisa iliyopita, baada ya kusindwa kutwaa taji
hilo ilipotinga fainali mwaka 2012 kwa kufungwa na Yanga SC mabao 2-0.
Mchezo huo wa fainali unatarajiwa kuanza saa
9:45 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki, huku mchezo wa kusaka mshindi wa
tatu ukitarajiwa kuanza saa 7:30 mchana ukizikutanisha timu za Khartoum ya
Sudan dhidi ya KCCA kutoka nchini Uganda.
Post a Comment