![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiuemSzTUoKYNi-0Cx1nyyPsq1RJo5cYaZCXHasG853L-jARoL7MjT-G2mCDjOvp43Y1z0LHOwmtB3g1tKD4moPNwR_6dCi2Ks1gzDtyRRYGdB3IJvSHNF9k_6UPGqwQQzfLcS20osYyQM/s400/Mourinho_Wenger_he_3394228b.jpg)
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
ameingia tena kwenye headlines kwa kauli zake anazozitoa kuelekea mchezo wa
Ngao ya Hisani,
Chelsea itakutana na Arsenal August 2 saa 11
jioni kwenye uwanja wa Wembley wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 90,000.
Mourinho ambae anajulikana kwa kuwa na uwezo wa kucheza na akili ya
kocha wa timu pinzani amerudi na kauli nyingine dhidi ya Wenger.
“Sifikirii
kuhusu nini kilitokea nyuma, nafikiria kuhusu mechi mimi kushinda mechi sita,
saba, nane au tisa bila kupoteza mechi hata moja haiweki utofauti wowote na
sifikiri kama itasaidia chochote kwenye huu mchezo, mechi inayofuata kwangu
haina mahusiano yoyote na mechi iliyopita
Kocha wa Arsenal
Arsene Wenger hajawahi kuifunga klabu ya Chelsea hata mara moja
ikiwa chini ya Jose Mourinho, wachambuzi wa masuala ya soka wanatafsiri
kauli za Mourinho kama ni njia ya kumdanganya kocha wa Arsenal Arsene
Wenger ili ajiamini zaidi.Mourinho amekuwa na rekodi nzuri dhidi ya
kocha wa Arsenal kwani akiwa na kikosi cha Chelsea amewahi
kucheza na Arsenal mechi 12 na kushinda mechi saba na kutoka suluhu
mechi tano hivyo hiyo ni sababu inayoendelea kumtia jeuri.
Post a Comment