Kocha wa klabu ya Manchester City Manuel Pellegrini bado ana endeleza harakati zake za kusaka taji la Ligi Kuu Uingereza linaloshikiliwa na klabu ya Chelsea kama bingwa mtetezi, August 16 timu hizo zimekutana na kucheza mchezo ambao umevuta hisia za walio wengi katika Uwanja wa Man City Etihad.
Bado hali sio nzuri kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Uingereza Chelsea, August 16 Man City imevunja rekodi ya Chelsea kwani katika mechi zake 28 zilizopita za Ligi Kuu Uingereza Chelsea haijawahi kupoteza mchezo hata mmoja ila goli la dakika ya 31 la mshambuliaji wa Argentina Sergio Aguero lilianza kuikatisha tamaa Chelsea.
Mchezo umemalizika kwa klabu ya Man City kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 3-0 magoli ya kifungwa na Sergio Aguero dakika ya 31, Vicent Kompany dakika ya 79 na goli la mwisho likifungwa na Fernandinho dakika ya 85, hii ni wiki ya tatu mfululizo Chelsea kutopata matokeo mazuri kwani ilifungwa na Arsenal katika mechi ya Ngao ya Hisani baada ya hapo ikafuatia sare ya goli 2-2 na Swansea City.
Hizi ni picha za mechi mtu wangu
Hii ni video ya magoli mtu wangu
Post a Comment