Dk.
Magufuli alitoa ahadi hiyo jana, wakati akijinadi kwa wananchi wilayani
Nkasi na Kalambo, mkoani Rukwa akiwa katika siku ya pili ili
achaguliwe kuwa rais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka
huu.
Alisema Baraza lake la Mawaziri ni lazima liwe na tofauti kubwa kwani watakuwa watumishi wa watu na siyo mabosi wa watu.
Alisema
waziri atakayeteuliwa katika serikali hiyo, atampima na akiona hawezi
kutimiza majukumu yake ipasayo kwa wananchi, lazima aondolewe na nafasi
yake ichukuliwe na waziri mwingine mwenye kasi ya kufanya kazi kama
yake, vinginevyo atawafukuza kila mara.
Dk.
Magufuli ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ujenzi, alisema atafanya hivyo
kwa sababu wananchi wanataka matatizo yao yatatuliwe kwa wakati na si
kusubiri siku inayofuata.
“Baraza langu litakuwa la kutetea wanyonge, litafanya kazi za wananchi, nachukia uzembe na nitaonyesha kwa vitendo,” alisema na kuongeza kuwa serikali yake itahakikisha fedha zinapelekwa kwa wananchi kutekeleza miradi ya maendeleo.
“Ifike
mahali tunaadhimisha wiki ya maji na maji yapo, wiki ya nyama na nyama
zipo, wiki ya Ukimwi na dawa zipo na wiki ya maziwa na maziwa yapo,” alisisitiza.
Vilevile,
aliwaonya watendaji wazembe akisema hawana nafasi kwani mwendo wake
utakuwa ni wa mchakamchaka na hakutakuwa na mapumziko hadi maendeleo
yawafikie wananchi.
Mgombea
huyo aliahidi kuunda serikali isiyo na kero kwa wananchi wa ngazi zote,
wakiwamo wa kipato cha chini, na itakuwa mkombozi kwa mamalishe na
waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda kwa kuwa itahakikisha zinafikia
mwisho.
Kwa
upande mwingine, Dk. Magufuli aliahidi kuboresha mishahara na maslahi
mengine kwa madaktari na wauguzi ili kudhibiti wizi wa dawa za serikali
na kuziuza kwa wagonjwa kwenye maduka yao na kusababisha hospitali,
vituo vya afya na zahanati kukosa dawa.
“Tunataka hospitali na zahanati zetu ziwe na dawa za kutosha, mwananchi apate huduma nzuri,” alisema.
Kadhalika,
alisema serikali yake ina mpango wa kujenga zahanati katika vijiji
vyote, vituo vya afya kwenye kata, hospitali wilayani na hospitali za
rufaa mikoani ili kusogeza huduma za matibabu karibu na wananchi na
kuwaondolea kero ya kusafiri kufuata huduma hiyo mbali na makazi yao.
Dk.
Magufuli aliahidi kuwa akiingia madarakani baada ya kuchaguliwa,
kitaumbele cha kwanza kitakuwa ni kutoa elimu bure kuanzia darasa la
kwanza hadi kidato cha nne huku akiwataka Watanzania kuzaliana kwa wingi
kwa kuwa serikali itabeba jukumu la kusomesha watoto wao.
Alisema fedha za kutekeleza hilo zipo kwa kuwa atakuwa amedhibiti mafisadi na wezi wa mali za umma.
Post a Comment