BAD
news! Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekumbwa na
masaibu mapya ya kuvamiwa na vibaka nyumbani kwake, Mbezi Beach jijini
Dar na kumuibia simu zake mbili aina ya Iphone.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni
ambapo wezi hao wanadaiwa kuruka ukuta na kufanikiwa kuvunja dirisha la
chumba anacholala mrembo huyo na kumliza simu hizo huku yeye akiwa
amelala fofofo.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wezi hao
walitumia mbinu za ‘kisayansi’ kutekeleza zoezi lao kwani siku hiyo Lulu
alirudi nyumbani mapema na akawa anachati kwa kutumia moja ya simu
hizo, ghafla akapitiwa ambapo alikuja kushtuka na kukuta dirisha
limevunjwa na simu zimetoweka.
“Nimemhurumia sana Lulu kwa kuwa siku
ambayo ameibiwa, simu kesho yake tena akafiwa na bibi yake mzaa mama
ambaye ndiye alikuwa kipenzi chake sana. Hapo utagundua alipata majanga
kiasi gani maana wakati alikuwa bado anafikiria ishu ya simu huku tena
akakumbana na janga la kifo.
“Amelazimika kutafuta simu nyingine anayoitumia sasa tofauti na awali alikuwa nazo mbili,” kilisema chanzo hicho.
Paparazi wetu baada ya kupenyezewa ubuyu
huo, alimtafuta Lulu ili aizungumzie ishu hiyo, ambapo alikiri kufikwa
na masaibu hayo huku akishindwa kufafanua zaidi juu ya tukio hilo kwa
kile alichodai alikuwa sehemu yenye kelele.
“Ni kweli nimepata matatizo sana mwezi
huu ikiwa pamoja na hilo la kuibiwa simu, sema kwa hapa nilipo siwezi
kuzungumzia lolote maana nipo katikati ya watu wengi na kuna makelele
sana. Lakini itakuwa vyema nikikutafuta baadaye,” alisema.
Licha ya Lulu kutotaja kiasi, simu hizo zinakadiriwa kufikia kiasi cha shilingi milioni tatu.
Licha ya Lulu kutotaja kiasi, simu hizo zinakadiriwa kufikia kiasi cha shilingi milioni tatu.

Post a Comment