Jumanne wiki hii baada ya waandishi wa
habari kuzuiwa kuingia katika chumba cha kuchukua fomu kwenye Ofisi za
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dar kwa kile ambacho viongozi wa Ukawa
walisema ni ukosefu wa hewa kutokana na udogo wa chumba, ilianza
minong’ono kuwa afya ya Lowassa labda siyo.
Lakini Ofisa Habari wa Chama cha
Wananchi (Cuf), Silas Bwire alipoulizwa juu ya hilo alisema madai hayo
ni propaganda za wapinzani wao kisiasa kwani afya ya kiongozi huyo iko
vizuri.
“Kwanza watu wanatakiwa wajue afya si
mali ya mwanadamu, ni mali ya Mungu, binadamu haupaswi kumhukumu
mwenzako kuhusu afya yake, wakati wewe mwenyewe hujajua kitu gani
kinatokota tumboni mwako,” alisema Bwire.
Alisema Lowassa ana afya nzuri ndiyo maana anaendelea na mapambano ya kwenda ikulu.
Wakati huohuo, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, Salum Mwalimu alisema hali ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe aliyefikishwa hospitali hapo Jumatatu ya wiki hii imeimarika na kwamba tatizo lake lilisababishwa na uchovu tu.

Post a Comment