Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KINANA ATUPA KOMBORA LINGINE KWA LOWASSA.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amesema kwamba chama Chama Mapinduzi kinatarajia kupata ushindi mnono katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwezi oktoba mwaka 2015.
Akizungumza na Wanachama wa CCM leo katika ofisi ndogo za CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es salaam mara baada ya mgombea wake wa Urais Dk.John Pombe Magufuli kuchukua fomu ya kugombea urais tume ya Taifa ya Uchaguzi  amesema kwamba chama hicho kwa bahati nzuri mwaka huu kinashindana na makapi yake ambayo kamwe hayawezi kuishinda CCM.

“Nchi yetu inakwenda kwenye uchaguzi ikiwa na wagombea na makapi, sasa kati ya mgombea na makapi nani mshindi?” Amehoji  Kinana

Ameongeza kuwa kila mwanachama akitengwa na CCM mahala pake ni wapi? Huku mamia ya wananchi wakijibu ‘Chadema’ kwa sauti ya juu.

Naye Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya Kikwete amesema kwamba  serikali ya CCM imefanya mambo mengi ya Maendeleo na mwaka huu wana waahidi watanzania ushindi wa kishindo.

Kwa upande wa Mgombea Urais wa CCM Dk. John Magufuli amesema kwamba ikiwa atachaguliwa kuwa rais  anakwenda kufanya wananchi walicho mtuma kwa kuwa shida za watanzania anazifahamu huku akirejea kauli yake Maendeleo hayana chama.

Hivi karibuni chama cha Mapinduzi kimepata mtikisiko mkubwa kufuatia  wanachama wake kuhama chama hicho na kutimkia Upinzani hususani Chama cha Chadema akiwemo Waziri mkuu wa Zamani Edward Lowassa, Makongoro Mahanga, James Lembeli  pamoja na Ester Bulaya
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top