Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Nuh Mziwanda Ajibu Tuhuma za Kumtongoza Wema Sepetu


Baada ya kusambaa sauti ya Nuh Mziwanda akimtongoza Wema Sepetu, muimbaji huyo ameibuka na kukanusha kuwa sauti hiyo sio yake na kumtuhumu Wema kuitengeneza sauti hiyo.

Akizungumza na mtandao  wa  Bongo5  akiwa na mpenzi wake Shilole, Nuh amesema kitendo kilichofanywa na Wema pamoja na timu yake sio cha kistaarabu.

“Mimi nimetake easy, ni mambo ya dunia kwa sababu ni mambo ya dunia ambayo yapo duniani. So wameamua tu kufanya vile sio suala ambalo lipo na sio suala sahihi,” amesema Nuh.

“Ile sio sauti yangu watu tu wameamua kufanya ili kunichafulia mimi labda na mpenzi wangu. Kwa sababu ukisikiliza mwishoni kuna mtu amejitaja jina lake. Ni kitu ambacho kimepelekwa studio wakaiweka sawa ili wapate kitu kibaya kije kwangu na Shishi. Hiki kitu sikukitegemea kwa sababu watu waliofanya kitu kama hicho ni watu ambao kwenye vitu vingi, kwenye mambo ya kampeni yaani mimi sijategemea,” ameongeza.

“Mimi hili suala nalichukulia kawaida na naona ni ushamba na upu*vu na hawana akili hata kidogo. Kama ni kweli, angemfuata Shishi akamwambia kwamba ‘mpenzi wako kafanya kitu fulani fulani kwangu’ sio kutangaza. 
 
"Na kama kweli, kwanini asingesema wengine wanaomtongoza na akawaweka mtandaoni? Ni Wema pamoja na watu wake wote ndio wamefanya hivi! Siku ya kwanza Shishi alilipokea vibaya lakini baada ya kumuelewesha kanielewa,” amesisitiza.

Kwa upande wa Shilole amekiri kulipokea jambo hilo kwa mshtuko lakini tayari ameshamsamehe Nuh na maisha yanaendelea.

“Mimi sina ugomvi na mtu katika maisha yangu,” amesema Shilole. 
 
“Kama wametengeneza ili wafanye hayo yote mimi sijali, watajua wenyewe, of course limeathiri mapenzi yetu. Sasa hivi tupo fresh, kwasababu mwenyewe ameshaniomba ‘mpenzi wangu samahani kwa kilichotokea lakini sio kweli.’ Nimeshamsamehe, mimi nimemuelewa alichosema Nuh basi.”
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top