
Meneja
wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amesema kuwa kiungo wa klabu yake Jack
Wilshere anatarajiwa kurejea tena dimbani wiki mbili zijazo baada ya kupata
maumivu ya kifundo cha mguu.
Wilshere
mwenye miaka 23 aliumia katika mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya Agosti 1
ambapo ilidhaniwa angekaa nje ya uwanja kwa miezi miwili. Lakini Wenger amesema
kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza anatarajiwa kupona ndani ya muda mfupi
ujao.
Wakati
huo huo mchezaji mwenzake Tomas Rosicky aliyefanyiwa upasuaji wa goti
anatarajiwa kukaa nje ya dimba kwa miezi miwili. Akiongea kabla ya kukutana na
Crystal Palace katika mchezo wa jumapili, Wenger alisema ''Jack atakua nje kwa
wiki nne na tiyari zimepita wiki mbili anaendelea vizuri''
Kiungo
Rosicky mwenye miaka 34 aliumia mwezi juni alipokua akiitumikia timu yake ya
Jamhuri ya Czech iliyomenyana na Iceland katika michuano ya kufuzu Euro 2016.
Post a Comment