|CCM wahaha kutafuta mgombea mbadala.
|Zitto Kabwe aingia makubaliano na CCM.
Yale yaliyotabiriwa kwa muda mrefu kwamba chama cha ACT Wazalendo (chini ya kiongozi Mkuu Zitto Kabwe) ni Mpini wa CCM kumaliza upinzani nchini, HATIMAYE YAMETIMIA. Habari zilizopo ni kwamba kumetokea sintofahamu kubwa ndani ya Chama Cha ACT Wazalendo baada ya aliyetarajiwa kubeba bendera ya chama hicho kwa tiketi ya Urais, Profesa Kitila Mkumbo kuamua kupingana na viongozi wenzake ndani ya chama hicho na kukataa kuwa msaliti wa vuguvugu la mabadiliko linaloendelea kufagia siasa za Tanzania, hasa baada ya Edward Lowassa kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA huku mgombea huyo wa UKAWA (Edward Lowassa) akiendelea kukipa Chama cha mapinduzi (CCM) mgombea wake John Magufuli wakati mgumu kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.
Hatua ya Profesa Kitila Mkumbo kuamua kukataa kuwa msaliti wa vuguvugu la mabadiliko yanayotakiwa na wananchi walio wengi imetishia uwezekano wa chama cha ACT Wazalendo kukosa mgombea wake wa Urais.Kutokana na hali hiyo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kuingilia kati na kusisitiza kwamba ni lazima ACT Wazalendo isimamishe mgombea wake kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba. Lengo kuu ni kuhakikisha kwamba ACT Wazalendo inapunguza kura za Ukawa (Lowassa) huku kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akiwa tayari ameshaingia katika makubaliano na CCM kutekeleza mradi huo.
Kwahiyo wakati wowote kuanzia sasa, ACT Wazalendo itamtangaza mgombea wake wa urais na sasahivi kazi ya kumpata mgombea huyo wa Urais (ACT Wazalendo) inasimamiwa na Chama Chama Mapinduzi (CCM).
Kwa karibia miaka miwili sasa kumekuwepo na mjadala mkubwa humu Jamiiforums kuhusu jinsi gani chama cha ACT Wazalendo chini ya Zitto Kabwe kimekuwa kinatumiwa na Chama Tawala (CCM) Kama mpini wa kumaliza upinzani nchini. Hatimaye yametimia, na Mjadala wa kina juu ya jinsi gani tumefika hapa unapatikana kwenye uzi wa Nguruvi3 kwa kubofya hapa:
Duru za siasa: Chama cha ACT -Wazalendo Mpini wa CCM kumaliza upinzani
MODS, tafadhali msiondoe au kuunganisha uzi huu na mwingine kwani katika mazingira ya sasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, uzi huu unajitegemea, lakini muhimu zaidi, utasaidia umma kuelewa jinsi gani CCM inajaribu kila njia kuhujumu UKAWA kuelekea Oktoba 25.
Chanzo: Mchumbuzi Kutoka Jamii Forums
Post a Comment