CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema hakipo tayari kujiunga na Ukawa kama ambavyo habari za uvumi zimekuwa zikizagaa katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa chama hicho kipo mbioni kujiunga na Ukawa.
Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe
jana na kusema kuwa taarifa zinazoenea kuwa chama hicho kitajiunga na
Ukawa sio za kweli.
"Leo( jana ) siku nzima nilikua nina kikao cha mashauriano na viongozi wa chama wa kata zote za mkoa wa Dar es salaam ( mikutano mikuu ya majimbo 10 ya Dar) jumla ya wajumbe 1023 walihudhuria, tumesisitiza kuwa hatutajiunga UKAWA…
"Ikumbukwe kuwa tuliomba utaratibu wa kujiunga UKAWA mwezi Aprili mwaka 2015 na hatujajibiwa rasmi lakini moja ya chama ndani ya UKAWA kilitangaza kuwa hawatutaki.
"Hata juzi kwenye gazeti la Mawio waliandika kuwa tumefukuzwa UKAWA, sisi tumeamua kuingia kwenye uchaguzi wenyewe..
"Tarehe 10 Agosti 2015 tutatangaza mgombea Urais tutakayemuunga mkono baada ya mkutano mkuu wa kidemokrasia wa ACT Wazalendo.
"Tutanadi #AzimioLaTabora kama zana ya kuleta mapinduzi katika nchi yetu," alisema Zitto Kabwe

Hivi karibuni kumekuwepo na tetesi kuwa chama cha ACT Wazalendo kipo
katika mchakato wa kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ili
kuongeza nguvu umoja huo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25
mwaka huu.
Post a Comment