Blue amepost picha Instagram akiwa na mke wake huyo na kuandika,” Morning ig…@wahyda_bysers_heart …siwezi kuelezea jinsi gani nampenda mke wangu….##kumekucha#lifeisgud.”
Hivi karibuni Mr Blue byser alitangaza hadharani kuwa sasa sio mfuasi tena wa vilevi vya aina yoyote, na ashukuriwe mke wake kwa kuwezesha hilo. Kupitia akaunti yake ya Instagram, hit maker huyo wa ‘Pesa’ alikiri kuwa sasa ana furaha zaidi baada ya kufanikiwa kuacha kuvuta bangi, sigara (fegi) mirungi na pombe. Alimshukuru mama mtoto wake kwa kumwezesha kuacha kutumia vilevi hivyo.
Hiki ndicho aliandika Blue:
“Alhamdulilahi ..nimeamka salama nikiwa mwenye furaha ahsante mungu ..na nashukuru pia kwa kufaulu mtihani ahsante mke wangu@wahyda_bysers_heart kwa kunifanikisha kuacha vilevi vyote..(bangi, fegi, mirungi, pombe) na kuishi km binadamu wa kawaida..nawashauri ndugu zangu kuwa makini na marafiki wengine wapo kwa ajili ya kukuharibia maisha yako ..kuwa makini… “
Post a Comment