Hatua hiyo imefikiwa baada ya wajumbe wa NEC wa Zanzibar wanounda kamati maalum ya Zanzibar kukutana hapa Zanzibar katika ofisi kuu ya CCM na kuamua kumuidhinisha Dr Shein kugombea tena kiti hicho cha urais baada ya wajumbe karibu 102 ambao ni aslimia 83 kuridhia Dr Shein agombee.
Awali Dr Shein ambaye ni makamu mwenyekiti wa CCM Zanzibar alilazimika kuondoka ndani ya kikao ili ijadaliwe na wanachama hao ambapo kiti hicho kilishikwa kwa muda na Dr Mohamed Gahribu Bilali makamu wa rais, ambapo baadaye akizumgumza na wanaccm hao waliokubali Dr Shein aliwahidi wanachama wa CCM kuwa uamuzi wake uko palepale wa kutekeleza ilani ya CCM ya kuitumikia Zanzibar.
Katika hatua nyengine naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar akizungumza baada ya kikao hicho alisema CCM haiwezi kupinga au kukubali suala la majimbo,wao wanasubiri maamuzi ya tume na wako tayari kwa umauzi wowote utakaotolewa na tume ya uchaguzi ambayo inatarajiwa kutangaza majimbo mapya leo asubuhi.
Kupitishwa kwa Dr Shein kugombea urais wa Zanzibar na kamati maalum ni hatua ya kwanza na sasa shuguhli yote inahamia Dodoma ambapo jina la Dr Shein litajadiliwa na kamati kuu na baadaye kutakiwa kuidhinishwa na kupitishwa na halmashuri kuu ya CCM, nafasi ya urais wa Zanzibar inaamuliwa na NEC na siyo na mkutano mkuu waccm.
Post a Comment