KHA! Kuna madai kwamba, Aunt Ezekiel alishaandikiwa talaka na ipo nyumbani kwa wazazi wa aliyekuwa mumewe, Sunday Demonte, Temeke Mwisho jijini Dar.
Muingizaji wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
Kwa mujibu wa chanzo, talaka hiyo iliandikwa na mumewe huyo baada ya
kupata taarifa kwamba, mkewe huyo ana ujauzito unaodaiwa kuwa ni wa
Mnenguaji wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moze Iyobo.“Hivi mnajua kwamba, Aunt alishaandikiwa talaka? Kama hamjui mjue sasa. Ipo Temeke kwa wakwe zake. Jamaa si yupo Uarabuni mahabusu, alisikia mkewe ana mimba ya Iyobo. Nadhani wanashindwa kumpa hiyo talaka kwa sababu walishakata mawasiliano naye tangu kitambo,” kilisema chanzo.
Aunt mwenyewe alipotafutwa juzi na kuulizwa kuhusu madai hayo, alisema:
“Sijui lolote kuhusiana na hilo, aliyesema kuwa nimeandikiwa talaka ipo ukweni kwangu ndiye angesema kila kitu yeye kwa vile anajua, mimi sijui.”
Post a Comment