Msichana mmoja mrembo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja hivi karibuni alifanya kitendo cha aibu baada ya kunaswa akimchomolea simu Mwanamuziki Raheem Rumy Nanji ‘Bob Junior’.Tukio hilo la kushangaza lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Bills Posta jijini Dar, ambapo Bob Junior alikuwa miongoni mwa wasanii waliokuwa wakipafomu.
Mrembo huyo akimpiga simu Mwanamuziki Raheem Rumy Nanji ‘Bob Junior’.
Awali, paparazi wetu alimuona mrembo huyo akipanda jukwaani na
kuonekana kama aliyekuwa na lake jambo lakini alipofeli alishuka. Mara
ya pili demu huyo alipanda tena, safari hii alifanikiwa kumkumbatia
msanii huyo lakini katika hali ya kushangaza alionekana akihangaika
kuzama mfukoni mwa Bob Junior na kuichomoa simu kiulainiii.Tukio hilo liliwafanya watu waliokuwa wakimkodolea macho kupiga kelele za; Unaibiwa simuuu…unaibiwa simuuu…, kitendo kilichomfanya msichana huyo kuirudisha mfukoni simu hiyo fasta kisha kushuka.
Baada ya tukio hilo mwandishi wetu alijaribu kuongea na Bob Junior ambapo alisema. “Mimi awali sikujua kama naibiwa lakini yale makelele ndiyo nikashituka, yaani yule demu bwana angeondoka na ile simu ingekuwa balaa.”
Post a Comment