Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akipungia mkono wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, alipokuwa akiondoka ofisi za chama hicho wilaya ya Shinyanga mjini mara baada ya kupata wana CCM wa kumdhamini .
Mh. Lowassa amabaye yuko kanda ya ziwa kutafuta wadhamini, jana amevunja rekodi ya kupata wadhamini 7,114, idadi ambayo ni kubwa kuliko mgombea mwingine yeyete ndani ya CCM hadi sasa.
Furaha ya kumuona Mh. Lowassa, ilitawala ukumbi mzima
Wana CCM waliofika kumdhamini Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, wakishangilia wakati akiingia ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Juni 11, 2015.
Wananchi wa mkoa wa Shinyanga, wakisukumana ili wapate kumuona Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, alipokuwa akiwasili kwenye ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini Juni 11, 2015, ili kuomba wanachama wenzake wa chama hicho wamdhamini.
Post a Comment