Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

HII NDIO HATMA YA SAMATTA KUCHEZA SOKA ULAYA….

samatta_cska_2Wakala wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta, Jamal Kisongo amesema hatma ya mshambuliaji huyo kucheza soka la kulipwa Ulaya sasa itasubiri mwakani kutokana na rais na mmiliki wa klabu yake yake TP Mazembe Moise Katumbi kuonesha bado anahitaji huduma yamchezaji huyo hususan katika michuano ya vilabu bingwa barani Afrika.
“Katumbi ameonesha bado anahitaji kumtumia katika kikosi chake kwenye michuano ya champions league kwa maana hiyo makusudio yetu na matarajio yetu, kunatimu moja kubwa ilitaka kumsaini kwa ‘Euro’ milioni moja lakini bahati mbaya Katumbi alitaka amuache baada ya champions league kuisha”, amesema wakala huyo wa Samatta.
“Kwahiyo hili tulilitazama kwa upande wetu na kuona si jambo la busara kama ni biashara hiyo ni bora abaki tu mpaka Januari ili aweze kuondoka kama mchezaji huru na yeye kuweza kufaidika zaidi kama mchezaji na si kuinufaisha TP Mazembe”, amesema.
“Kwa kawaida, huwa sio vizuri sana kuviweka hivi vitu wazi, kwasababu ni mapema, lakini kwa hiyo timu waliokuwa wanataka kutoa kiasi hicho cha pesa ilikuwa siyo klabu ya Ulaya, ilikuwa ni klabu moja kubwa ya Afrika. Na hicho ndio kitu kimojawapo kilichochangia kukataa ofa hiyo, kwasababu kusudio letu kubwa lilikuwa ni kuhakikisha kwamba Samatta anacheza mpira Europe”, amefafanua.
“Sisi tunataka hata kama pesa itakuwa ndogo lakini aende akacheze soka Ulaya na kufungua milango kwa wenzake hata kama pesa ni ndogo. Tunauhakika kama ataweza kucheza Ulaya kwa mwaka mmoja, basi anauwezo wa kutengeneza pesa nyingi na timu kubwa zitakuwa zimeshaingia kwenye vita kubwa ya kumsaka”, ameeleza.
“Tumeshapokea ofa nyingi zaidi ya sita timu hasa zinamuhitaji, anahitajika na timu nyingi. Tumepokea ofa kutoka Uswis, Ufaransa, Hispania na maeneo mengine. Ni mchezaji ambaye yupo kwenye soko la Ulaya na timu zinamuhitaji”, alimaliza
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top