Kwa nini sakata la Ufujaji umeme wa dharura la kampuni ya Richmond liliolazimu kupangwa upya baraza la mawaziri linazungumzwa kwa nafasi kubwa na wanasiasa hadi sasa, huku ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali-CAG zinazoibua ubadhirifu mkubwa kila mwaka zikisahaulika kirahisi?
Kama
waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa asingehusishwa na sakata la
Richmond kwa namna washindani wake kisiasa wanavyolazimisha,
sakata lingeendelea kuzungumzwa?
Maswali
haya mawili yana majibu yake sahihi kwa wanaojua undani wake,
akiwemo Lowassa aliyejiuzulu ili kulinda heshima na mustabali
wa nchi, serikali na chama cha mapinduzi-CCM, kama anavyonukuliwa
akisema. Yawezekana amelinda maslahi ya nchi kwa vile wahisani
hawakusitisha misaada yao muhimu kwa bajeti ya nchi.
Kwa
muktadha wa makala na ulinganifu wenye mantiki, hakuna manufaa
makubwa kwa umma kupigia kelele Richmond iliyopitia Dowans na
kubaki Symbion Power na kujisahalisha huu ubadhirifu na upotevu
mkubwa wa fedha za umma unaobainishwa kila mwaka na CAG bila
kufanyiwa kazi ipasavyo kwa hatua stahiki dhidi ya wahusika.
Hizi
mbinu za kisiasa za kukumbuka Richmond ili kutimiza malengo
ya baadhi ya wanasiasa ya kulazimisha na kuwaaminisha watu
mambo yawe watakavyo yanazidi kufifia na kushindwa kadri siku
zinavyozidi kubadilika.
Eti wanakumbuka sana Richmond kwa vile imehusishwa na Lowassa!!!
Sina
nia ya kumsafisha mchafu yeyote wala kumchafua msafi bali
nauzungumzia uhalisia tu.Unawezaje kukumbuka Richmond na kukataa
kuona ubadhirifu unaoibuliwa na CAG anapoonyesha zaidi ya sh.
trion moja zimeyeyuka serikalini?!
Kama
ilivyokuwa Richmond na waliouaminisha umma iwe watakavyo katika
bunge la kasi na viwango la Spika Smweli Sitta ndivyo
ilivyotokea kwa sakata la Tegeta Escrow ambapo wanasiasa
wamethubutu kutoa hukumu wanayolazimisha iwe dhidi ya wale
walioitwa mafisadi, na kuimiminisha dhana husika kwa wananchi.
Baadhi
ya wahusika waliojiuzulu kutokana na sakata la Esrow kama njia
ya kuonyesha uwajibikaji kisiasa wamethibitika kutohusika. Kati
yao ni aliyekuwa waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter
Muhongo na katibu mkuu wake Eliakim Maswi, ambao kamati maalumu
iliyoundwa kuchunguza uhusika wao haikuona hatia yoyote dhidi
yao.
Bahati
mbaya, enzi za Richmond hakukuwa na kamati maalumu ambayo
ingethibitisha, kwa mfano, usafi wa wanasiasa waliohusishwa na
Richmond baada ya kujiuzulu kwao.
Sijui
wanasiasa wanaoshupalia Richmond wakidhani kuikumbuka kwa
kutaathiri safari ya kisiasa ya Lowassa wakiambiwa ukweli
tofauti watatumia kete gani mpya kujipandisha kisiasa.
Wanasiasa
wenye "homa ya Lowassa" wanaamini kete pekee ya kufifisha
umaarufu, kukubalika na safari ya matumaini ya Lowassa ni
kutumia sakata la Richmond.
Bahati
mbaya ya makusudi kwao ni kutowaambia wananchi ile Richmond
wanayojikumbusha hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu
octoba mwaka huu, ndiyo hii Symbion ambayo Rais wa Marekani
Barack Obama anaijua na anaamini kazi inayofanywa nayo ndani
ya Tanzania katika sekta ya Nishati.
Sasa
wewe mwanasiasa ukiikumbuka Richmond, unganisha Dowans ili
uiseme Symbion kwa sauti ya juu itakayowafikia wananchi ili
waweze kukuuliza umefanya nini au unakumbuka yapi angalau kimya
kimya kuhusu EPA,Kagoda,Meremeta,Deep Green Finance,Tegeta Escrow;
unachukuliaje ripoti mpya ya CAG na uamuzi wa wahisani
kusitisha misaada muhimu ya kibajeti kwa nchi.
Hadi sasa kunawatu hawako tayari kusikia tofauti na walivyoaminisha au kuaminishwa juu ya Richmond.
Pengine
ule msemo apendao kuutumia Rais Kikwete kwamba "Akili za
kuambiwa changanya na za kwako" ni muafaka kuwagutusha watu
ili wapambanue dhamira za wanasiasa kabla, wakati na baada ya
kusikia wanenacho na watendacho.
Endapo
wanasiasa watadhani siasa za kuchafua wagombea wanaotakiwa na
wananchi walio wengi ili wao wasiotakiwa wabahatike kuteuliwa
na vyama, yaliyomtokea Goodluck Jonathan na kilichokuwa chama
tawala Nigeria si ajabu kujirudia kwa CCM.
Post a Comment