Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

PIERRE NKURUNZIZA ATANGAZA RASMI KUGOMBEA URAIS

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza.
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza ametangaza rasmi azma yake ya kugombea kwa awamu ya tatu katika uchaguzi mkuu ujao nchini humo, licha ya kuendelea upinzani wa kila upande ndani na nje ya nchi hiyo wa kumtaka asifanye hivyo.
Rais Nkurunziza alitangaza rasmi azma yake hiyo jana Ijumaa na kuyataja maandamano ya wapinzani ambayo kwa mujibu wake yamegeuka kuwa uasi, kwamba atayamaliza hivi karibuni.
Aidha rais huyo kijana aliahidi kuandaliwa haraka iwezekanavyo mazingira bora kwa ajili ya kufanyika uchaguzi ujao.
Tayari Tume Huru ya Uchaguzi nchini Burundi imemtaja Rais Pierre Nkurunziza kuwa mgombea wa kwanza kusajiliwa katika tume hiyo kwa ajili ya kushiriki katika uchaguzi huo uliopangwa kufanyika tarehe 26 Juni mwaka huu.
Hii ni katika hali ambayo maandamano ya kupinga kugombea tena Rais Nkurunzinza yangali yanaendelea nchini Burundi huku wimbi la wananchi wa Burundi wanaokilimbilia nchi jirani za Tanzania, Rwanda, na DRC nalo likizidi kuwa kubwa.
CHANZO: IRAN SWAHILI
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top