Staa wa muziki Feza Kessy, ambaye hivi sasa amezindua track ambayo ni
kolabo yake na Chegge ya 'Sanuka', amefarijika kutumbuiza katika onesho
kubwa la muziki la Party In The Park lililofanyika jijini Dar.
Katika onesho hilo lilokusanya maelfu ya mashabiki na mastaa mbalimbali,
pamoja na kutumbuiza vyema stejini Feza aliwamwagia sifa wanamuziki
Sauti Sol, Mafikizolo na Ali Kiba ambao walitikisa na muziki wao wa
Live.
Feza ameiambia enewz kwamba amegundua kuwa kitu ambacho kinawafanya wasanii hawa nyota kuzidi kutambulika kimataifa ni kwa sababu ya kubakia katika asili yao kisanaa na hii ni kutokana na kujituma zaidi ili kufikia malengo yao kimuziki.
Aidha Feza amesema kwamba mipango yake ikikaa sawa anatarajia kufanya
kazi na nyota hao ambao kwa kiasi kikubwa amevutiwa nao sana, huku
akifurahi kuona wimbo wake wa 'Sanuka' kupokelewa vyema na mashabiki
wake akisema 'the future for Feza is brighter than bright, Watch Out
world.
Endelea kutazama EATV ambapo tutaendelea kukujulisha yaliyotokea katika onesho hilo lililofanyika wikend iliyoisha pale The Green Oysterbay Kenyatta Drive jijini Dar es Salaam, tukiwa moja ya wadhamini wa nguvu kabisa wa burudani hiyo ya kukata na shoka.
-EATV

Post a Comment