Huyu ndio mama aliyeibiwa mtoto wake Mei 8 mwaka huu huko mkoani Morogoro.
Mtoto huyo aliibiwa kimafia Mei 8, mwaka huu wakati mama yake Martha
Masawe akiwa kwenye foleni katika Kliniki ya Nunge mkoani hapa.Baada ya habari hiyo kuchapishwa Mei 10, mwaka huu, wananchi wa Kitongoji cha Mikumi Wilaya ya Kilosa mkoani hapa walimtilia shaka mkazi mwenzao Jesca Patrick (23) ambaye ghafla alionekana akiwa na mtoto mchanga mara baada ya kutoka Morogoro mjini wakati hawakuwahi kumuona akiwa na ujauzito.
Huyu ndo mama anaedaiwa kuiba mtoto ambaye alifahamika kwa jina la jesca.
“Waliposoma habari ya kuibiwa mtoto gazetini halafu ghafla wakaona
Jesca ana mtoto mchanga, wakamtilia shaka na kutoa taarifa polisi katika
Kituo cha Polisi cha Mikumi, akakamatwa,” kisema chanzo chetu.”Siwezi kubisha ni kweli nilifanya jaribio la kumuiba mtoto huyo kwani nilifanya juhudi za kuzaa lakini bahati mbaya mpaka leo sijabahatika kupata mtoto hivyo naomba mnisamehe,” alisema Jesca ambaye ni mkazi wa Mikumi.
Kwa upande wake Martha, alikuwa na haya ya kusema:
“Kwa kweli nalishukuru sana gazeti hili, yaani nilitamani nife kwa kumkosa mwanangu. Pia nalishukuru jeshi la polisi kwa kufanikisha kumpata mtoto wangu akiwa hai na afya njema na kumtia mbaroni mtu aliyemuiba,nimefurahi sana,” alisema Martha.
Post a Comment