Kocha wa klabu ya Arsenal, Mfaransa Arsene Wenger
amelalamika ukosekanaji wa mastraika wa kimataifa katika soko la wachezaji
Ulaya.
Wenger ambae kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na usajili
wa Karim Benzema kutoka klabu ya Real Madrid amesema kuwa yeye hawezi kusajili
mchezaji kwa gharama kubwa ilihali kiwango cha mchezaji huyo hakina tofauti
sana na viwango vya wachezaji ndani ya klabu yake.
“Mimi huwa sikatai kusajili pale ambapo ni wazi kuwa
mchezaji unayemsajili ana kiwango kikubwa na ataongeza ubora katika kikosi
chako. Tatizo ni pale tu unapotaka kutumia hela nyingi kusajili ilihali kiwango
cha mchezaji huyo hakina tofauti na viwango vya wachezaji wako. Sipo tayari kwa
hilo”
Kaui hiyo ya Wenger inapunguza matumaini ya arsenal kutaka kumsajili Benzema. Real Madrid tayari wameshaweka wazi kuwa thamani ya Benzema ni Uero millioni 45.
Post a Comment