Klabu ya Chelsea mpaka sasa imeshafungwa magoli matano ndani
mechi mbili za mwanzo katika ligi kuu Uingereza.
Kocha wa klabu hiyo, jose Mourinho tayari ameshawataja
wachezaji wa timu yake ambao anadai kuwa ndio wamekuwa aibu kwa timu yake hiyo
kupoteza mechi hizo.
Mourinho amesema “sijafurahishwa
na kiwango cha mchezaji yeyote. Sijafurahishwa na Hazard, Ivanovic, Terry, Azpilicueta,
Matic na Fabregas. Sina furaha nao kwa sababu nahitaji kupata matokeo mazuri Zaidi
ya haya ninayoyapata sasa”
Chelsea wanajiandaa na pambano dhidi ya West Brom wikiendi hii na tayari Mourinho anataka kikosi chake kirejee kwenye kiwango kizuri ili waendelee kupata ushindi.
Post a Comment