Mwanamuziki
wa miondoko ya mduara ambaye kwa hivi sasa anatumikia kifungo cha mwaka
mmoja kilichotolewa na Baraza la Sanaa Basata ya kutojihusisha na
shughuli za kisanaa kwa mwaka mmoja amesema ameumizwa mno na
adhabu aliyopewa na baraza hilo, hali inayomfanya afikirie
kutembea na waume za watu ili aweze kuyamudu maisha yake ya
kila siku
Akizungumza
na mwandishi wetu, Shilole alisema kuwa adhabu aliyopewa ni kubwa mno
kiasi ambacho anashindwa kuelewa kwa kuwa sanaa ndiyo kazi inayompatia
kula na hata kuwasomesha watoto wake hivyo kumfungia mwaka mzima ni kama
kumtuma kutembea hata na waume za watu ili maisha yake yazidi kusonga
mbele.
“
Mimi naona sasa wananituma kuanza kusaka waume za watu kwa kweli kwa
sababu mwaka mzima kweli na ni kazi ambayo naitegemea kwa kila kitu
katika maisha yangu kwa nini mtu usiwaze vitu vingine kama huna kazi ya
kufanya jamani, yaani inaniuma sana,” alisema Shilole.
Post a Comment