August 19 Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Borniface Wambura ametangaza ratiba rasmi ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara ambapo Ligi Kuu itaanza Septemba 12 wiki moja baada ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kucheza na timu ya taifa ya Nigeria mchezo wa kufuzu AFCON 2017.
Wambura
amethibitisha kupangwa kwa ratiba ya Ligi hiyo kwa kuzingatia mazingira
ya timu zinakotoka na sehemu zinakoenda ili kuvisaidia vilabu kupunguza
gharama za nauli, ratiba pia imepangwa kwa kuzingatia timu
zitakazoshiriki klabu Bingwa barani Afrika na kombe la shirikisho.
Hata hivyo Wambura alitangaza pia kuanza kwa kombe la FA
ambapo litashirikisha timu 64, timu 16 za Ligi Kuu, timu 24 za Ligi
daraja la kwanza na timu 24 za Ligi daraja la pili kwani ujio wa Kombe
la FA unakuja sambamba na neema ya kupatikana kwa mdhamini wa Kombe la FA.
Ratiba ya Kombe la FA
itatoka baada ya kutoka kwa ratiba za Ligi daraja la kwanza na Ligi
daraja la pili kwani timu shiriki zinategemea viwanja ambavyo pia
vitatumika katika michezo ya Ligi Kuu.
“Msimu wa
Ligi umeshafunguliwa kwa maana ya usajili ila kwa mashindano tutaanza
kucheza Septemba 12 na tutamaliza mzunguuko wa kwanza Novemba 7 baada ya
hapo tutaingia katika usajili wa dirisha dogo kupisha michuano ya
Challenge Cup na tutaendelea December 19 na tutaenda kumaliza Ligi Mei 7
2016″>>>Wambura
Hii ni ratiba yote ya Ligi Kuu
Hii ni sauti ya Wambura unaweza kumsikiliza
Post a Comment