Kitengo maalum cha Oparesheni
Fichua Moavu (OFM) cha Global Publishers wakiongea na mhudumu wa baa
moja iliyopo Ubungo External, Ilala jijini Dar .
Chande Abdallah na Deogratius Mongela
WAMENASWA! Kitengo maalum cha
Oparesheni Fichua Moavu (OFM) cha Global Publishers mwishoni mwa wiki
kiliwanasa wahudumu wa baa wakiuzwa kwa wanywaji wanaohitaji huduma ya
ngono katika mtego uliofanywa katika baa moja iliyopo Ubungo External,
Ilala jijini Dar es Salaam.
Awali, mtoa habari wetu alikiambia
kitengo hicho kuwa wako wahudumu wengi wa mabaa mbalimbali jijini Dar es
Salaam wanaojiuza na kwamba wanafanya hivyo kwa kuwa wanapata baraka
kutoka kwa viongozi wao (mameneja) ambao huwaruhusu kuondoka wakati
wowote wakiwa kazini kwa makubaliano ya malipo ya shilingi elfu mbili
(2000).
“Ukishalipa hiyo hela unaondoka naye na
huko sasa ndiyo mnapoelewana wenyewe kama mtalipana kiasi gani kabla ya
kufanya mapenzi, kifupi wengi wa wahudumu wa kwenye baa ni kama
machangudoa, ile kazi ni utambulisho tu,” kilisema chanzo hicho na
kuzitaja baa kadhaa jijini Dar zenye mtindo huo hasa za maeneo ya
Ubungo, Tandale, Buguruni, Tandika na Mbagala Rangi Tatu.
Wakiendelea kuongea na mhudumu huyo.
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, OFM
iliingia kazini na kuanza na baa moja maeneo ya Ubungo External, lakini
cha kushangaza, ilikutana na wahudumu wa kiume tu, ambao walisema wenzao
wa kike walikuwa wameondoka na wateja.
Katika baa ya jirani yake, OFM ilifika
na kuagiza vinywaji kama kawaida, kabla ya kuingia mzigoni kwa
kumtongoza mhudumu mmoja wa kike, ikitaka kuondoka naye muda uleule.
OFM: Mambo vipi?
BAAMEDI: Poa.
OFM: Njoo ukae hapa kuna jambo nataka kukueleza.
BAAMEDI: Mh! Siwezi kukaa, (huku akisogea na kumpa sikio Kamanda) haya niambie.
OFM: Nimevutiwa sana na wewe, naweza kukupata saa hivi?
BAAMEDI: Mh! Hapana, labda baadaye kwa sababu sasa hivi tuna wateja wengi, tupo bize sana.
OFM: Nitakupata muda gani?
BAAMEDI: Saa 4 hivi nitakuwa poa.
(alisema baamedi huyo huku akiondoka baada ya kuitwa meza nyingine).
Post a Comment