Kwenye maelezo ya picha yake ameandika’Kwanini Mimi,wewe na Yule tumuunge mkono MAGUFULI Oktoba 2015 kwa kumpa kura zetu.
- 1MAGUFULI ni muadilifu na mcha Mungu aliyepata malezi mazuri kupitia familia na kanisa Katoliki.
- 2. MAGUFULI ni msomi mbobezi katika sayansi hususani hisabati na
kemia.3. MAGUFULI ni kiongozi mwenye msimamo asioyumba hata kidogo.
4.MAGUFULI ni mtu wa kusimamia sheria,kanuni na utaratibu bila uwoga wala ubaguzi.
5. MAGUFULI ni mtu anayependa sana haki itendeke kwa kila anayestahili bila kupindishwa.
6. MAGUFULI ni mchapakazi na anayechukia uzembe.
7. MAGUFULI ni mtu aliyezaliwa katika familia maskini inayojishughulisha na kilimo cha pamba,uvuvi na ufugaji.
8. MAGUFULI ni mtu wa kufuatilia jambo mpaka matokeo chanya yapatikane. Si mtu wa kusubiri ripoti ofisini.
9. MAGUFULI ni kiongozi wa kipekee mbali na kuwa mbunge na waziri kwa miaka 20 watoto wake wote wamesoma shule za msingi za serikali ya Mbuyuni na shule ya sekondari ya Kata ya Makumbusho. Ana imani na shule zetu na anajua kero na matatizo yake.
10. MAGUFULI ni mtu anayechukizwa na kukerwa sana na rushwa. Amewahi kufukuza wafanyakazi 400 kwenye mizani za kupima uzito wa magari kwa rushwa kukithiri katika mizani na kuajiri wengine.
11. MAGUFULI ni mnyenyekevu sana na asiye na majivuno.
12.MAGUFULI ndiye waziri pekee katika serikali ya awamu ya nne aliye sifiwa sana na bunge wakiwemo wapinzani kuwa ni JEMBE na nchi ikimpata mtu wa aina yake itafika mbali sana.
13. MAGUFULI ni mtu anayependa kuongoza kwa kuonyesha njia. Katika wizara alizowahi kuziongoza katika miaka takribani 20 watumishi wake wanasema MAGUFULI amekuwa mtu wa kukutwa ofisini wakati wote na wa mwisho kutoka. Hii ilijenga nidhamu kwa watumishi wengi.
14. MAGUFULI hana deni na mtu. Jamaa hajatumia hata senti moja kuhonga wajumbe au kuunda timu wala kuchangiwa na matajiri hivyo atatutumikia kwa uhuru na haki akilinda maslahi ya nchi.
15. MAGUFULI ni mkali sana dhidi ya watendaji wazembe,wala rushwa,wabadhirifu na wavivu.
Post a Comment