FC Barcelona, Pedro.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania alitua kwa dau la £21.4million
baada ya uvumi wa muda mrefu kua atahamia Manchester United, lakini hali
ikawa tofauti na sasa yupo The Blues.
Pedro amesaini mkataba wa miaka minne ambao utambakisha kwa mabingwa hao wa Premier League mpaka mwaka 2019.
Baada ya kutia saini Pedro alisema "Nina furaha sana kua hapa. Nina
shauku ya kuonesha maajabu yangu Chelsea na kushinda vikombe.
"Asante kwa klabu na wadau mbali mbali kwa kuniwezesha kuvaa jezi ya blue"
Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa Ujerumani, TZ Online, tayari
Chelsea wametoa ofa kwa Bayern na PSG kwa ajili ya nyota wake, Willian
ikiwa ni hatua iliyochukuliwa kufuatia ujio wa Pedro.
Post a Comment