Tottenham
wako tayari kumnyatia mshambuliaji wa QPR Charlie Austin, 26, ambaye atagharimu
karibu pauni milioni 15 (Daily Mirror), Spurs pia wanatarajia kuwazidi kete PSV
na Atletico Madrid katika kumsajili winga kutoka Colombia Jeison Lucumi, 20,
anayechezea America de Cali ya daraja la pili (Daily Mail),
mshambuliaji mpya
wa Manchester United Memphis Depay, 21, amemuambia meneja Louis van Gaal kuwa
anataka kuvaa jezi namba 7 aliyokuwa akivaa Angel Di Maria (Telegraph), nahodha
wa Chelsea John Terry anaamini Chelsea itakuwa timu ya kwanza kutetea taji lake
mfululizo katika kipindi cha miaka saba (Evening Standard), Real Madrid
wanaweza kushawishiwa kumuuza Karim Benzima, 27, lakini Arsenal watalazimika
kuvunja rekodi yao ya uhamisho kwa kutoa pauni milioni 45 (Daily Mail), Asier
Illarramendi, 25, ameambiwa na Real Madrid kuwa hana nafsi ya kucheza katika
klabu hiyo msimu huu na hivyo huenda akafikiria kuhamia Liverpool (Daily
Express), Liverpool wanazungumza na Fiorentina kuhusu uhamisho wa Fabio Borini,
24 (Talksport), Angel Di Maria anatarajia kutangazwa rasmi kwa mashabiki wa
Paris Saint-Germain leo (Daily Star), beki wa kushoto wa Augsburg Baba Rahman,
21, amekubali kuhamia Chelsea, lakini bado timu hizo mbili hazijakubaliana bei
(Sky Sports), Manchester United wamepanda dau jingine kumtaka mshambuliaji wa
Tottenham Harry Kane (Daily Express), Nigeria imefanya juhudi za kumshawishi
nyota chipukizi wa Liverpool Jordon Ibe, 19, kuichezea timu ya taifa ya
Nigeria, badala ya England ambayo ameichezea katika ngazi ya vijana (Daily
Mirror), Sergio Aguero, David Silva na Samir Nasri, huenda wakakosa mechi za
mwanzo wa msimu baada ya kurejeshwa nyumbani kutoka mazoezini wakisumbuliwa na
tatizo la tumbo (Daily Star), mshambuliaji wa zamani wa Liverpool El Hadji Diof,
34, ambaye anaichezea klabu iitwayo Saba ya Malaysia amesema anataka kuingia
katika siasa atakapostaafu soka (Sun), uhamisho wa mkopo wa kiungo Leroy Fer wa
QPR kwenda Sunderald umeshindikana baada ya mchezaji huyo kutopita vipimo vya
afya (Independent), Saido Berahino huenda akasalia kuwa mchezaji wa West Brom,
baada ya klabu hiyo kusema haijasikia lolote kutoka kwa Tottenham waliokuwa
wakimnyatia (Birmingham Mail), mshambuliaji wa Manchester United Javier
Hernandez amepewa dau la dola milioni 10 na klabu moja ya ligi ya Marekani MLS,
na amepewa saa 24 kuamua hatma yake (NBC Sports).
Loading...
Home
» Sport
» HARRY KANE KUKIPIGA MANCHESTER UNITED, BENZEMA KUTUA ARSENAL MUDA WOWOTE : KUSOMA HABARI ZA USAJILI KWENYE MAGAZETI YA LEO BOFYA HAPA.
Post a Comment