Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Mwandishi wetu
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Diamond Platnumz’ amekubali kuwa yupo tayari kupokea mamilioni ya fedha
kwa ajili ya kumfanyia kampeni mgombea urais kupitia muunganiko wa
vyama vya upinzani Bongo vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), Edward Ngoyai Lowassa, Ijumaa limenyetishiwa.
LICHA YA URAFIKI NA JK
Habari za uhakika kutoka chanzo cha
kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa Diamond zilidai kwamba, licha ya
jamaa huyo kuwa na urafiki na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’ ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), lakini mbele ya mkwanja anaweza kuamua tofauti.
Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Diamond.
LOWASSA VS MAGUFULI
Chanzo hicho kilieleza kwamba, jamaa
huyo amekuwa akishawishiwa kujipambanua kuwa atamfanyia nani kampeni
kati ya Lowassa na Dk. John Pombe Magufuli wa CCM zitakazoanza Agosti
22, mwaka huu.
“Unajua hata kipindi kile wakati Lowassa
anatangaza nia Arusha, jamaa (Diamond) alikwenda kwenye shoo kwa sababu
ya mkwanja tu lakini ukweli ni kwamba alikuwa upande wa Bernard Membe
(naye alikuwa mtia nia wa CCM).
KWENYE MTONYO
“Unajua Dangote (Diamond) linapokuja
suala la mtonyo, huwa halazi damu. Ukweli anaomba Mungu tu mamilioni
yatue mikononi mwake maana yeye siyo mwanasiasa ni mfanyabishara kupitia
muziki.
“Anakwambia muziki ni biashara kama
biashara nyingine. Ni kama kuuza maji, haijalishi wewe ni chama gani
lazima utahitaji maji au huduma nyingine yoyote bila kujali siasa,”
kilidai chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa gazetini na kuongeza:
“Huo ndiyo msimamamo wa wasanii wengi,
Ukawa wakileta mzigo watapatiwa huduma yao na CCM nao wakija watapewa
huduma wanayohitaji. Ni kama siti ya daladala, haijalishi anayekalia ni
Chadema au CCM.”
KUTOKA NDANI YA UKAWA
Duru za kisiasa kutoka ndani ya Ukawa
zilidai kwamba, tayari fungu limetengwa kwa ajili ya wasanii
watakaozunguka na mheshimiwa (Lowassa) Tanzania nzima kwa ajili ya
kampeni.
“Diamond ni mmojawapo lakini wasanii
watakaokuwa bega kwa bega na Lowassa ni wengi. Kuhusu kama wameshasaini
mikataba hilo lipo wazi kwani time (muda) yoyote watadakishwa mamilioni
yao,” kilisema chanzo chetu ambacho ni mmoja wa wasanii walio ndani ya
Team Lowassa tangu akiwa CCM.
Rais
Kikwete akipokea CD mpya ya msanii Naseeb Abdul “Diamond” baada ya
kuoneshwa tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda, Ikulu jijini
Dar Desemba 23, 2014.
DIAMOND AFUNGUKA
Baada ya kunyetishiwa habari hizo,
gazeti hili lilimtafuta Diamond ili kujua kama ameshakabidhiwa mamilioni
hayo na kwamba anayazungumziaje?
Ijumaa: Mambo vipi Baba Tiffah?
Diamond: Poapoa. Inakuwaje?
Ijumaa: Princess Tiffah na mama’ke hawajambo?
Diamond: Wako poa sana, namshukuru Mungu, hapa nipo jikoni nawaandalia madikodiko, si unajua tena?
Rais
Kikwete akiongea na msanii Naseeb Abdul “Diamond” alipomkaribisha Ikulu
kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu,
Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne Desemba 23, 2014.
Ijumaa: Oke. Kwanza
hongera kwa sababu kuna habari imetufikia kwenye Dawati la Ijumaa
kwamba, umevuta mamilioni ya Ukawa. Hii ishu ikoje?
Diamond: Habari njema hizo. Sijasaini mkataba lakini nazingoja kwa shauku kubwa.
Ijumaa: Nasikia wanakutafuta sana hao Ukawa, je, umeshaongea nao?
Diamond: Mimi ni
mwanamuziki wa Tanzania, nina haki ya kwenda kumburudisha Mtanzania
yeyote ikiwa ametimiza hitaji la malipo yanayotakiwa kwa shughuli yake.
Haitakiwi Ukawa wala CCM kunilaumu kwa namana yoyote ninapokwenda kutoa huduma ya burudani.
Mimi napokea simu nyingi za biashara na mimi ni mfanyabishara, kwa nini dili likija nisilichukue? Dili lije nalisubiria.
URAFIKI WA DIAMOND NA JK
Mara kadhaa Diamond amekaririwa akisema
kuwa JK ni rafiki yake mkubwa akimwita Daddy ndiyo maana humtembelea
mara kwa mara ikulu hivyo kwa kuwa ni Mwenyekiti wa CCM anaweza
kumshawishi msanii huyo kuzunguka mikoani kumpigia kampenzi mgombea wake
ambaye ni Magufuli.
Post a Comment