Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais. Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetukama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande.
Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010. Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach.
Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi. Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala. Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
Post a Comment