Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Tukio la Kituo cha Polisi Kutekwa: Viongozi Wa Dini Wacharuka.......Wamtaka Rais Kikwete Afanye Mabadiliko ya Jeshi la Polisi

VIONGOZI mbalimbali wa dini nchini wameandaa maandamano  kwa lengo la kumuona Rais jakaya kikwete ili kumuomba alifanyie mabadiliko makubwa Jeshi Polisi.

Mabadiliko hayo ni pamoja  na kubadili mawaziri  wote wa mambo ya ndani,  mkuu wa jeshi hilo (IGP)  na  MA-CP wawili ambao wametajwa  kuendesha jeshi hilo  kimtandao  kinyume  na taratibu za kijeshi.

Maandamano hayo yamefikiwa na Maaskofu na Mashekhe 160 wa mjini Dodoma jana chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya  Maadili, amani na haki za binadamu ya Madhehebu ya Dini Nchini Askofu William Mwamalanga.

Mwamalanga alisema  viongozi hao wamepokea taarifa ya kuuwa  kwa  askari polisi  wanne wa kituo cha stakishari cha jijini Dar es Salaam  kwa masitikito.

“Tumepokea taarifa ya vifo vya askari hawa kwa masikitiko, hali hii haikubaliki kila mara vituo vimekuwa vikivamiwa na hadi sasa takriban Askari 47 wameuwawa,” alisema Mwamalanga.

Huku akibubujikwa na machozi ya Uchungu Askofu Mwamalanga amehoji ukimya wa  Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe na IGP Erinest Mangu kwa vifo vyote ambavyo vimekuwa vikitokea tangu mwaka huu uanze.

“Uvamizi huu na mauaji ya askari wa chini unatisha   na hatuoni hatua yoyote ya maana  iweje wahalifu wawe na nguvu kuliko jeshi hasa kipindi hiki ambacho dunia inakabiliana  na makundi ya wahalifu hatari wakiwemo al shabab,” alihoji.

Kufuatia hali hiyo, ASkofu  Mwamalanga  amemuomba  Rais kikwete  kuwaongeza askari  wangazi ya  chini  mishahara   kwa kiwango cha Millioni moja ili  walingane na wenzao wa  nchi za afrika mashariki na kusini.

Alisema hatua hiyo itawawezesha askari hao kukabiliana na changamoto za maisha kama  ilivyofanya kwa wafanyakazi Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ambapo ilisema hiyo itawaondolea tamaa za Rushwa.

“Kwa Polisi ni zaidi kwani kitendo cha kuuwawa kama tembo porini bila mshahara mzuri kunawakatisha tamaa na ari ya kufanya kazi,” alisema.

Askofu  Mwamalanga  ambaye ni Mwanaharakati  Mtafiti wa haki  za jamii  alisema idadi kubwa ya Maaskofu na Maashekhe nchini wamelaani Mauaji  hayo yanayoendelea dhidi ya polisi.

“Tayari zaidi ya askari 47 wameuwawa na wengine wamebaki vilema, silaha  lukuki zimechukuliwa vituoni na kutokomea kusikojulikana, hili lina dhihirisha kuwa Taifa letu lipo pabaya. Ndiyo maana tunaona ipo haja tena muhimu kwa rais kwachukilia hatua za haraka  wanaosababisha uzembe huo ikiwa ni pamoja na kulifanyia ukarabati jeshi hili,” alisema.

Aliwakumbusha watanzania kuliona jeshi hilo kuwa ni chombo chao cha kuwalinda  wao wawe salama dhidi magenge ya uhalifu  duniani hivyo wana wajibu kama  raia wema  kuhakikisha wanawalinda askari  hao kwa hali na mali ikiwa ni pamoja na kuwapa taarifa muhimu ili kuwakamata  wauaji wote pamoja  na silaha zote zilizoporwa.

Aidha  viongozi hao  walihoji kuondolewa kwa vizuizi [ berial] barabarani kulikuwa na maslahi gani kwa usalama wa nchi kwani hivi sasa  wahalifu  wametumia nafasi kutoroka kirahisi pale wanakuwa wamefanya uhalifu.

“Tunataka vizuizi hivyo virudishwe mara moja kwa barabara zote nchini,” alisema.

Kwa upande wake shekhe  Athumani Mukambaku   ambaye ni  Mwenyekiti mwenza wa Kamati  hiyo  na mjumbe wa BAKWATA halmashauri ya mkoa wa dar es Salaam alishauri serikali itunge sera mahususi ya  raia  wote kuwalinda  polisi  baadala  ya dhana iliyojengeka kuwa ni polisi pekee ndiyo wenye wajibu wa kulinda  raia, jambo linalojenga chuki pale ambapo  polisi wanaposhindwa  kusimamia haki za raia sawasawa.

“Katika kipindi hiki cha kulelekea uchaguzi mkuu jeshi linapaswa kuimarisha vituo vyake vyote ikiwa ni pamoja na kufunga kamera maalumu za cctv ili kuweka rekodi ya watu wote wanaotembelea vituo hivyo pamoja kuvunja kanda maalumu za kipolisi ambazo hazionesha juhudi ya kupambana na uhalifu na baadala yake zimeongeza gharama  kwa jeshi  hilo,” alisema Shekhe Mukambaku.

Alisema rais anapaswa ateue makamanda wabunifu wanaokwenda na wakati na kwamba  kila mkoa uwe maalumu kwa kuimarisha vitendea kazi vya askari ikiwa ni pamoja kuwapatia  motisha wale walio ngazi ya chini ambao hukesha  vituo kuimarisha ulinzi.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top