Minong’ono! Tumbo la staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ limezua maswali kwa wadau kibao kama ni la kawaida au tayari mwandani wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Muziwanda’ ameshampachika ujauzito.
Shilole au Shishi Baby alizua minong’ono hiyo wikiendi iliyopita nyumbani kwa mwigizaji, Aunt Ezekiel Grayson maeneo ya Mwananyamala jijini Dar ambapo kulikuwa na shughuli ya 40 ya mtoto wa Aunt, Cookie iliyokwenda sambamba na futari huku mastaa kibao wakijumuika katika tukio hilo.
Akiwa kwenye tukio hilo, Shilole alizua maswali baada ya tumbo lake kuonekana limejaa kama mjamzito.
“Dah nipo kitambo sasa lakini sijapata picha kama tumbo la Shilole ni mimba au kashiba tu, maana kwa uzoefu wangu jinsi anavyoonekana atakuwa na mimba,” alisema mmoja wa mashuhuda.
Baada ya kuona hali hiyo, mwanahabari wetu alimfuata Shilole kwa lengo la kumtaka azungumzie ishu hiyo kama ni tumbo tu au ameshanasa ujauzito, ambapo alisema:
“Ni kweli nina mwanaume rijali lakini sijabahatika kupata mimba, nadhani muonekano wa tumbo ni kwa sababu ya nguo niliyovaa ila natamani kupata mtoto,” alisema Shilole.
Post a Comment