MBUNGE anayemaliza muda wake, Salvatory Machemli, amekuwa Mbunge wa kwanza wa jimbo kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kubwagwa kwenye kura za maoni zinazoendelea ndani ya chama hicho.
Machemli,
aliyekuwa Mbunge wa Ukerewe mkoani Mwanza, alijikuta akishindwa kupata
kura za kutosha katika uchaguzi huo uliofanyika juzi mjini Nansio,
Ukerewe.
Awali,
uongozi wa Chadema Makao Makuu ulikuwa na mapendekezo kwamba wabunge wa
majimbo wa chama hicho wapite bila kupingwa na ingawa wengi walikuwa na
wapinzani, wamefanikiwa kuvuka kizingizi cha kura za maoni isipokuwa
Machemli.
Aliyembwaga
Machemli ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Joseph Mkundi,
aliyepata kura 232 kati ya 466 zilizopigwa, akiwashinda wagombea wengine
tisa huku Machemli akiambulia kura 74.
Hata
kabla ya matokeo kutangazwa, tayari Machemli aliondoka ukumbini na
taarifa ambazo hazikuthibitishwa jana zinasema kwamba jana alikuwa
‘akiendesha operesheni’ maalumu ya kuwanyang’anya pikipiki wapambe wake
kadhaa aliowapa wamsaidie kufanya kampeni.
Post a Comment