Wadadisi wa mambo wamekuwa na maswali yasiyojibiwa hasa kuhusu ULAZIMA wa kuhakikisha Lowassa anapitishwa na chama chake kwa gharama zozote. Swali lingine ni tija ya projekti nzima kwa Watanzania...
Je waliohusika na mradi huu wanarandana na haiba ya mtu wao? Hapa nazungumzia watu kama Apson, Kingunge, Rostam, Chenge, Nchimbi n.k.
Je chaguo la Watanzania ni chaguo lao? Au chaguo lao ndilo chaguo la Watanzania?
Udadisi hauishii hapo bali plan B ya Wezesha Lowassa na utiifu wa kundi lake kwake nk.
Tambo za Lowassa kuwa hakuna wa KUMKATA jina lake kwenye hatua zote za mchujo, ni wazi kuna egemeo thabiti la ndani ya chama alilokuwa amejiaminisha kwake. Inawezekana mtaji wa wajumbe wa NEC na hamasisho la wajumbe wa mkutano mkuu, inawezekana vilimpa imani kuwa ana kundi kubwa linalomuunga mkono.
Tangu mteule wa CCM kupatikana, Lowassa amekuwa kimya kumuunga mkono au kukosoa mfumo uliofikisha utimilifu wa mchakato mzima. Hivyo haiyumkiniki plan B inaweza kuleta kishindo ama maumivu zaidi.
Shamrashamra, majivuno na tambo za mashabiki wa Lowassa ambapo walithubutu kutumia CCM kama kichaka chao hata kukiuka taratibu, kanuni na maadili ya Chama kwa kigezo cha kupendwa vimegeuka simanzi na fadhaa nzito kwao.
Hakuna tofauti na msiba kugeuka matanga na historia haibadilishwi...
Post a Comment