Msanii wa bongo movie Batuli ameweka wazi kuwa alikimbia kundi la Kaole sanaa Group baada ya kukutana na changamoto nyingi ikiwepo changamoto ya rushwa ya ngono.
Batuli alifunguka hayo Jumatano alipokuwa katika kipengele cha Kikaangoni kinachofanyika kila siku ya Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wa EATV.
Batuli
alifunguka na kusema kuwa moja ya sababu kubwa ambayo ilimfanya
kuondoka katika kundi hilo ilikuwa kuombwa rushwa ya ngono ili aweze
kupewa kipaumbele zaidi kuliko wasanii wengine jambo ambalo kwa upande
wake hakuwa tayari kulifanya na kuamua kuondoka katika kundi hilo.
Batuli
anasema kabla ya kuweza kutoka kupitia mkono wa Kanumba alishasota sana
katika kundi hilo na alikuwa akibaniwa nafasi kutokana na kutokubaliana
na watu ambao walikuwa wakimtaka kingono ili waweze kumpa kipaumbele
zaidi, ndipo hapo alipoamua kuondoka na baadaye msanii Kanumba ndipo
alipoamua kumpa nafasi na kuweza kumtoa kisanaa.
"Nilijiunga
kaole lakini baadae Kanumba aliniona nafaa kwenye filamu chini ya
kampuni ya Game 1st Quality ndivyo nilivyotoka ila kabla ya hapo
nilisota sana kwa sababu ya changamoto mbalimbali ikiwepo kubaniwa kazi,
na kutakwa kimapenzi au kuombwa rushwa ya ngono.
"Moja ya jambo lililofanya niondoke Kaole ni changamoto ya rushwa ya ngono, nilikutana na changamoto hiyo nilipojiunga na kikundi cha kaole nikaamua kuhama kikundi kabisaa"
"Moja ya jambo lililofanya niondoke Kaole ni changamoto ya rushwa ya ngono, nilikutana na changamoto hiyo nilipojiunga na kikundi cha kaole nikaamua kuhama kikundi kabisaa"
"Nilijiengua kaole baadae Kanumba alinishika mkono" Aliongeza Batuli
Mbali
na hilo Batuli alisema kuwa kwa sasa yeye ni mtalaka na ana watoto
wawili na katika kipindi chake cha ndoa hakuwahi kuchepuka hata siku
moja sababu huwa anapenda kutulia na mtu mmoja, na kuweka wazi kuwa
katika maisha yake hajawahi kugombanisha wanaume sababu huwa anapenda
kuwa na mtu mmoja anayempenda.
"Hapana
haijawahi kutokea nimegombanisha wanaume au wanaume wamegombana kwa
sababu yangu kwa kuwa huwa sina mahusiano mengi natulia na mmoja"
Tunatambua
katika tasnia ya filamu na movie nchini wasanii wengi wamekuwa
wakitumia kiki na skendo mbalimbali kama njia ya kujitangaza na
kujiongezea umaarufu zaidi katika sanaa husika jambo ambalo kwa Batuli
limekuwa kinyume chake.
Yeye anaamini kuwa skendo na kiki zinamfanya msanii adharaulike na kushusha heshima ya msanii huyo jambo ambalo yeye ameweza lifananisha na vazi baya au chafu katika tasnia ya filamu na sanaa kiujumla.
Yeye anaamini kuwa skendo na kiki zinamfanya msanii adharaulike na kushusha heshima ya msanii huyo jambo ambalo yeye ameweza lifananisha na vazi baya au chafu katika tasnia ya filamu na sanaa kiujumla.
"Sio
kweli, huwezi kuheshimika na scandals kuna mfanya msanii adharaulike
kila aendapo. Naweza kusema scandals ni vazi baya na chafu kwenye tasnia
yetu"
Post a Comment