Hata hivyo, nimetafakari sana juu ya hatma ya Lowasa na nimebaini kuwa anasumbuliwa na mambo yafuatayo;
1. JINSI YA KUREJESHA FEDHA ZA WAFADHILI WAKE
Lowasa ametumia kiasi kikubwa cha fedha tangu aanze mchakato wa kwenda Ikulu, vyanzo vyangu vimebaini kuwa Lowasa ametumia zaidi ya shilingi bilioni 50 hasa kuanzia mwaka 2012 alipojitokeza hadharani kuchangia huduma za kijamii, mashirika ya kidini, watu binafsi na taasisi mbalimbali. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 30 zimetumika kwa kipindi cha 2014 hadi alipokatwa rasmi Julai 9. Inaelezwa kuwa kiasi kingine cha fedha kipo mikononi mwa watu na kingine hakijulikani kimeenda wapi ijapokuwa bill imeenda kwa Lowasa. Hiki ni kiasi kikubwa cha fedha. Ni fedha ambazo alipewa kwa wafadhili wake kwa mategemeo kuwa zitarejeshwa baada ya yeye kwenda Ikulu ambapo walikubaliana kuwa watapewa miradi ya serikali. Hata hivyo, baada ya kukatwa, Lowasa hana namna tena ya kurejesha fedha hizo. Baadhi ya wafadhili wake kama akina Karamagi, Rostam, Manji na Reginald Mengi wameanza kumnunia na kwamba tangu juzi, baadhi yao hawajapiga hata simu kumsalimia tofauti na hapo awali ambapo kila mara walikuwa wanapiga simu kujuliana hali na kubadilishana mawazo. Jambo hili linamtatiza sana Lowasa.
2. HATMA YA MAISHA YAKE BAADA YA KUKATWA.
Lowasa alikuwa na uhakika wa asilimia 100 kuwa ndiye Rais ajaye. Ubongo wake aliutune usipokee aina nyingine ya maisha tofauti na majukumu ya mkuu wa nchi. Kitendo cha kukatwa hata kabla ya kuingia tano bora, hakika kinamnyima raha sana.
3. KUKIMBIWA NA WATU WALIOKUWA KARIBU NAYE.
Baadhi ya watu ambao mara zote walikuwa karibu naye inasemekana kuwa wamemkimbia. Miongoni wa watu hao ni pamoja na Emmanuel Nchimbi, Hamisi Mgeja, Jerry Slaa, Sophia Simba, Adam Kimbisa, Apson Mwang'onda, Mohamed Abdulaziz, Kingunge Ngombale Mwiru, Msukuma na wengineo wengi. Eneo ambalo amepoteza watu wengi ni kanda ya ziwa ambako aliwekeza fedha nyingi. Hakika kitendo cha watu hao kumkimbia ni pigo kubwa sana kwake. Sasa anakumbuka msemo wa kiswahili kwamba mgaa gaa namupwa hali wali mkavu. Kumbe waru wale hawakuwa na mapenzi mema kwake na kilichokuwa kinawapeleka ni fedha zake tu. sasa bahari imekauka wameamua kuikimbia lwani na kwenda kuishi bara.
4. MATAMSHI YA BAADHI YA WAFUASI WAKE KUMUUNGA MKONO MAGUFULI.
Baadhi ya wafuasi wake wamenukuliwa wakitoa matamshi ya kumuunga Mkono Mgombea wa CCM, JOHN POMBE MAGUFULI. Miongoni mwao ni Emmanuel Nchimbi ambaye ndiye alimuandaa kuwa Waziri Mkuu wake. Watu hao wamesikika wakisema kuwa hawana budi kumuunga Mkono Magufuli kwa vile anauzika kuliko wagombea wengine waliochukua fomu. Maneno hayo yamemkasirisha sana Lowasa na yanaendelea kumtesa kila akisoma kwenye mitandao ya kijamii. Ina mana yeye Lowasa hauziki?
5. WANACHAMA WALIOMDHAMINI WAKATI WA KUOMBA RIDHAA YA CHAMA
Lowasa alipata wadhamini zaidi ya laki nane na hivyo kuwa kinara kuliko wagombea wengine. Mgombea aliyepata wadhamini wachache, Magufuli ndiye kaibuka kuwa mshindi. Hilo linamtesa sana Lowasa. Kinachomsumbua zaidi ni zile pesa alizotumia kuwapa wadhamini hao. Lowasa anajua kuwa wadhamini hao wanajua siri hiyo na wakati wowote wataiweka hadharani. Ikiwa siri hiyo itawekwa hadharani, ni wazi kuwa ataendelea kuumbuka na hata kama atahama chama, huko atakakoelekea hatakuwa wa maana tena.
Kuna orodha ya mambo mengi sana yanayomtesa Lowasa. Hata hivyo, kukaa kimya anaona kuwa siyo suluhisho kamili. Njia anayoona muafaka ni ile aliyotumia awali. Yaani kuitisha press conference na kutoa ya moyoni. Yaani kati ya wagombea wote 38 waliorejesha fomu, huyu pekee ndiye anayeteseka baada ya kukatwa. Wengine wametulia tulii na wamekubaliana na matokeo. Hata hasimu wake kisiasa Benard Membe na hata Sammuel Sitta wameamua kukaa kimya na kutokuwa waropokaji. Wameheshimu maamuzi ya vyombo halali vya chama vilivyoundwa kwa kazi hiyo. Kazi ya KUKATA waliochukua fomu kwa vile masharti ni kwamba kuwe na wagombea watano tu wanaoenda NEC.
Kwa kumalizia, nawakumbusha Msemo wa JK kwamba UKITAKA KULA KUBALI NA WEWE KULIWA. Ndicho kinachomtesa hasa Lowasa. Kala sana vya watu na sasa anahofia kuliwa. Anajua kuwa watu kama akina Karamagi, Manji, Rostam hawatakubali kuona fedha zao zimeteketea. Lazima zirudi kwa njia yoyote ile.
JF...
Post a Comment