Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Watanzania tumwombee na tujitokeze kumsaidia mwanamuziki Banza Stone kwani yupo katika hali mbaya

Akizungumza katika kipindi cha jioni cha E-FM kinachoongozwa na Gadner G. Habash mama mzazi na kaka wa damu wa mwanamuziki fundi na bora wa kizazi cha kati cha watanzania Ramadhani Masanja a.k.a mwalimu wa walimu / Banza stone wamesema kuwa mwanamuziki huyo sasa ni siku ya tatu " hatoi kauli " na " hataki tena kunywa dawa " na " hali yake sasa inazidi kudhoofika " hali inayopelekea wao kukata tamaa na kumwachia mwenyezi mungu. 
Hata hivyo mama mzazi wa banza stone aliwashukuru sana wafanyakazi wa kituo cha redio cha e fm na msanii mwenziye muumini mwinjuma kwa kuwa wamekuwa bega kwa bega kujitokeza mara kwa mara kumtembelea na kumsadia mwanamuziki huyo mahiri ambaye binafsi nakiri kuwa huyu jamaa hakika ni " fundi " ktk medani za uimbaji na utunzi na hili halina ubishi.
Kinachonisikitisha sana ni kwamba hata wanamuziki wenzake tu ni kama vile wamemsusa mwenzao ukiachilia mbali huyo muumini mwinjuma na inasemekana kuwa hata wakipigiwa simu hawapokei na wengi wao wanajifanya wapo busy kwenye ma concert yao wakati ukweli ni kwamba wengi wao tunao humu humu mjini.
Hasira yangu kubwa ipo kwa wale mapedeshee wa mjini ambao nakumbuka walikuwa wakimfuata banza stone na kumpigia magoti kuwa awataje katika nyimbo zake kwa mfano " papa antibiotique muzee wa jamii forum mutu ya fedha mingi " ( wakati ukweli hata hizo hela sina ) lakini sasa hata kumsikia tu huyu jamaa aliyekuwa akiwafagilia hawataki na wanamkwepa.
Uchungu wangu mwingine naupeleka kwa marafiki zake ambao wakati ameugua mara ya kwanza na kupata nafuu ndiyo walikuwa wa kwanza kwenda kumchukua na kumpeleka kula nae bata huku wakimpa mipombesigarana powder huku wao wakidhani kuwa wanamsaidia kumbe ndiyo wamemfikisha hapa alipo sasa.
Jazba zangu za mwisho nazielekeza kwa wanahabari wa tanzania ambao nina uhakika wengi wao wameweza sana kutengeneza majina yao kupitia mgongo wa banza stone haswa kwa kupata habari zenye mvuto kutoka kwake na nakumbuka kuna tv nyingi sana zilikuwa zinamtumia banza stone kama chambo chao ktk kuvutia watazamaji wao lakini sijaona mwandishi yoyote aliyediriki hata kumpa coverage banza stone juu ya hii hali yake mbaya ya kiafya.
Hitimisho:
Najua wengi sasa tunasubiria tu kwa hamu labda Israeli afanye yake kwa Banza stone ili sasa tuanze kushindana kuvaa sutimadela,miwani huku tukienda na magari yetu ya kifahari msibani, kujifanya ku pledge mahela mengi huku tukitafuta coverage ya kutosha ktk media kwa kujifanya tunamjua sana banza stone na kutoa machozi ya kinafiki nakizandiki.
Chonde chonde watanzania wenzangu hali yaBanza stone ni mbaya....narudia nimbaya......na namalizia kusema kuwa nimbaya na naomba uzi wangu huu umguse kila mtu na tujitokezeni kwenda kumjulia tu hali na tuache ushamba kuwa kwenda kumwona mgonjwa ni mpaka uende na kitu ila kwenda kwako tu na maneno yako ya hekima,utu na busara kwa Banza stone kunaweza kumsaidia na akarudi katika hali yake ya kawaida.
Ewe Mwenyezi Mungu mpe nafuu na mjalie afya njema mwanamuziki wetu kipenzi Ramadhani Masanja (Banza stone ) kwani bado tunamujhitaji katika tasnia hii ya muziki wa dansi. 
Amina / Amen.
Nawasilisha..
Source: Jamii forums
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

www.7x24hours.blogspot.com
© Copyright 24hours
Back To Top