Brighton Masalu
UBABE? WASANII katika tasnia ya filamu, Irene Paul ‘Smart Girl’ na Halima Yahaya ‘Davina’ wamejikuta wakitaka kuzichapa kavukavu baada ya kushindwa kudhibiti hasira walipokuwa wakitaniana.
Irene Paul Ishu hiyo ilitokea juzikati ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, kulipokuwa na mkusanyiko wa wasanii mbalimbali ndipo wawili hao walipotunishiana misuli.
Halima Yahaya ‘Davina’ Ishu hiyo iliibuka baada ya Davina kumtupia maneno ya kejeli mwenzake huku Irene akionekana kuwa ‘siriaz’ akitahadharisha kuwa hapendi utani na kuanza kumtupia maneno makali jambo lililowafanya baadhi ya wasanii kutuliza hali ya hewa.
Mwandishi wetu aliyeshuhudia tukio hilo mita chache na mahali alipokuwa, alishuhudia Davina naye akimpa maneno makali mwenzake ndipo wakataka kuzichapa lakini bahati nzuri wakaamuliwa.
Post a Comment