Mkuu wa jeshi la wanahewa la Colombian amesema tukio hilo ni la maajabu.
''Kwa hakika hatujawahi kuona mtu ameishi baada ya ajali mbaya kama hii''alisema Kanali Hector Carrascal.
Bi Murillo alikuwa na majeraha madogo huku mwanawe akionekana kuwa na afya nzuri.
Bi Maria Nelly Murillo, 18, na mwanawe wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja walipatikana siku 5 baada ya ndege ya Cessna waliokuwa wakisafiria kuanguka katika msitu mkubwa ulioko katika jimbo la Choco.
Bi Murillo alikuwa na majeraha madogo huku mwanawe akionekana kuwa na afya nzuri.
Ndege hiyo yenye injini mbili ilikuwa ikisafiri kutoka Quibdo, hadi mji wa Nuqui iliyoko kwenye pwani ya Pacific kabla ya kuanguka siku ya jumamosi.
Hadi kufikia sasa haijulikani nini kilichosababisha ajali hiyo.
Hadi kufikia sasa haijulikani nini kilichosababisha ajali hiyo.
Kundi la waokoaji waliofika katika eneo la ajali walimpata rubani wa ndege hiyo akiwa ameaga katika chumba cha rubani.
Hata hivyo milango ya ndege hiyo ilikuwa wazi na abiria waliokuwemo hawakuwepo.
Kundi la waokoaji lilianza shughuli ya kuwatafuta na baada ya siku tatu wakawapata bi Murillo na mwanawe.
Walipelekwa Hospitalini
Kwa hakika ni Muujiza mkubwa kuwapata wakiwa hai''alisema Kanali Hector Carrascal.
Walipelekwa hospitalini kwa matibabu mjini Quibdo.
Post a Comment