UCHUNGU wa mwana si aujuae mzazi? Sasa mama mzazi huyu vipi?! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanamke Pendo Mabuko amejikuta akipokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira waliokerwa na kitendo chake cha kumtupa barabarani mwanaye wa kumzaa baada ya kunyimwa matumizi ya mtoto huyo na mwanaume aliyezaa naye, Daniel ambaye ni mume wa mtu.
Mtoto anayedaiwa kutupwa na mama yake, Pendo Mabuko.
Tukio hilo lililojaza umati lilitokea Ijumaa iliyopita, saa 10 jioni katika Mtaa wa Simu ‘A’ Kata ya Mji Mpya mkoani hapa. Wakihojiwa na gazeti hili, mashuhuda wa tukio hilo, Asha Hussein, Mussa Juma na Paskal Msimbe kwa nyakati tofauti, walisema:
”Tukiwa hapa barabarani tulimshuhudia huyu mwanamke na mwanaume mmoja wakizozana kwa muda mrefu, tulipowasogelea ili kuwasuluhisha, mwanaume alipanda bodaboda na kutimka.
“Ndipo huyu mwanamke akamtupa mtoto kisha naye akaanza kuondoka huku akisema amechoka kumlea mtoto wa mtu, sisi tukamzuia.
Mwanamke huyo akilia baada ya kupokea kichapo kikali kutoka kwa wananchi waliokelwa ha kitendo hicho.
“Tulimlazimisha kumchukua mwanaye lakini aligoma, tukaamua tukuite wewe mwandishi kwa msaada zaidi.”Wakati mwandishi wetu anawasili eneo la tukio, aliwashuhudia baadhi ya wananchi wenye hasira wakimshushia kichapo mwanamke huyo kwa kitendo cha kumtupa mwanaye.
Mwandishi aliita polisi wa pikipiki ambapo Afande Mwajabu alifika fasta na kumchukua mwanamke huyo na mwanaye na kuwapeleka kituoni kwa mahojiano zaidi.
Awali, akihojiwa na mwandishi wetu kuhusu uamuzi wa kumtupa mtoto wake barabarani, mwanamke huyo alisema:
”Muda huu tunatoka Ustawi wa Jamii kusuluhishwa. Mimi nilipeleka malalamiko, mzazi mwenzangu kagoma kumtunza mwanaye na kuniachia mzigo peke yangu.
Mama huyo akiwa mikononi mwa polisi.
“Nikimuuliza anasema mkewe kamzuia kumtunza mwanangu ndiyo maana na mimi kwa hasira nikaamua kumtupia mwanaye akamlee na mkewe.”
Post a Comment