Kocha Rafa Benitez baada ya kutua Real Madrid.
KLABU ya Real Madrid imemthibitisha Kocha Rafa Benitez kuwa meneja wao mpya baada ya kutimuliwa kwa kocha Carlo Ancelotti.
Zinedine Zidane (kushoto), ambaye ni kocha wa timu B ya Madrid akisalimiana na Benitez.
Benitez amesaini mkataba wa miaka mitatu kukinoa kikosi hicho
akitokea Napoli inayoshiriki Serie A iliyomaliza ikiwa nafasi ya tano.
Kocha huyo mwenye miaka 55, raia wa Hispania atatambulishwa kwa wanahabari leo.
Benitez alianza kazi yake ya ukocha katika klabu hiyo ya Madrid miaka
20 iliyopita na atatambulishwa kwa wanahabari leo Jumatano.
Post a Comment