Omotola Jalade , nyota wa filamu wa Nigeria ambaye amefikisha miaka 20 katika tasnia hiyo na kuwa alama ya fahari ya tasnia ya filamu ya Nollywood ya Nigeria, ametoa ya moyoni kuhusu kinachomfanya asitetereke kwenye ndoa yake ambayo imempatia watoto wanne.
Omotola Jalade akiwa na mumewe Mattew Ekeinde.
Kipenzi huyo cha mamilioni ya wapenda filamu duniani, akijulikana kwa jila la utani la Omosexy, amesema mumewe, Kapteni Mattew Ekeinde, ndiye kila kitu kwake na kwamba ndiye mtu pekee anayeweza kumdhibiti.
“Sidhani ningekuwa nimeolewa hadi sasa kama nisingeolewa mapema, kwani naona hakuna mtu awezaye kunidhibiti zaidi ya mume wangu. Si kwamba mimi ni mkorofi, bali nina msimamo imara. Sifahamu nini kinawafanya wasanii wengine wa kike kutopata wanaume sahihi wa kuishi nao,” alisema katika mahojiano hivi karibuni na gazeti la Vanguard.
Alisema wasanii wanapopata mafanikio wanachanganyikiwa na kushindwa kufahamu watu wanaowapenda kwa dhati kwa vile wanajiona wako matawi ya juu. Hii huwaletea matatizo wao wenyewe.“Mimi nimebarikiwa, nimefanya uamuzi wa makusudi bila kumwathiri mtu mwingine. Ni kwa vile ni uamuzi wa asili. Nina bahati kwa vile Mungu alinifundisha jinsi ya kutumia akili yangu,” alisisitiza mwigizaji huyo.
Post a Comment